MBOWE ATANGAZA KUSITISHA MIKUTANO YA CHADEMA KUKABILIANA NA CORONA | MALUNDE 1 BLOG

Monday, March 23, 2020

MBOWE ATANGAZA KUSITISHA MIKUTANO YA CHADEMA KUKABILIANA NA CORONA

  Malunde       Monday, March 23, 2020

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kupitia kwa Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, kimetangaza kusitisha kufanya mikutano yake ya hadhara nchi nzima, kama kilivyokuwa kimetangaza na badala yake kitaungana na Taifa katika kupambana na janga la ugonjwa wa Virusi vya Corona.

Akizungumza leo Machi 23, 2020, Jijini Dodoma, Mbowe amesema kuwa wakati anatoa kauli yake ya kutangaza uwepo wa mikutano ya hadhara kwa nchi nzima, Serikali haikuwa imetangaza uwepo wa mgonjwa yeyote wa Virusi vya Corona na kwamba wataendelea na mikutano yao pale ambapo hali ya ugonjwa huo itakuwa imetengemaa.

"Na moja ya ushauri uliotolewa ni pamoja na kuzuia mikusanyiko mikubwa mikubwa, kwahiyo sisi tutaahirisha shughuli zote hizo za mikusanyiko mikubwa ndani ya chama chetu na tutashirikiana na Watanzania wenzetu kuchukua tahadhari ili kuhakikisha kwamba tunaweza kupambana kikamilifu na janga hili la Corona" amesema Mbowe.

Aidha Mbowe ameiomba Serikali ione ipo haja ya kufunga mipaka yake yote ili kuhakikisha hakuna mgeni yoyote anayeingia nchini kutoka kwenye Mataifa yaliyoathirika na Virusi vya Corona.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post