BUNGE LASITISHA UTARATIBU WA KUPOKEA WAGENI ILI KUKABILIANA NA VIRUSI VYA CORONA


Bunge la Tanzania limesitisha utaratibu wa kupokea wageni mbalimbali wakiwamo wanafunzi wanaokwenda bungeni kwa lengo la kuona na kujifunza shughuli za Bunge.



Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Machi 19, 2020 na kitengo cha mawasiliano na uhusiano wa kimataifa cha ofisi ya Bunge imesema hatua hiyo ni mikakati ya muhimili huo uliotangazwa na Spika Job Ndugai wa kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa corona.

Taarifa hiyo imesema wageni watakaoruhusiwa kuingia bungeni ni wale wenye kazi na vibali maalum tu.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527