BENKI YA CRDB YAZINDUA MPANGO MAALUMU WA KUWAWEZESHA WANAWAKE KUSHIKA NAFASI ZA UONGOZI


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa tatu kulia) akiwakiwaonyesha wakurugenzi wengine wa Benki hiyo, moja ya tuzo zenye jumbe mbalimbali, wakati wa uzinduzi wa program maalumu ya kuwawezesha Wanawake (Mentoring Program for empowering Women) ili waweze kushika nafasi mbalimbali za uongozi, iliyofanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Johari Rotana, jijini Dar es salaam jana.

******
Benki ya CRDB imezindua mpango maalum wa kuwawezesha wafanyakazi wanawake katika nyanja mbalimbali ili  waweze  kushika nafasi za uongozi.

Akizindua mpango huo katika hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela alisema, Mpango huo ni mahususi katika kuwawezesha wanawake wa CRDB Banki ili waweze kuwa viongozi katika nyanja mbalimbali pamoja na kuwafanya waweze kujiamini na kukamata fursa zilizopo.

Mpago huo ni mwendelezo wa maadhimisha ya siku ya Wanawake Duniani, ambapo Benki ya CRDB imeamua kuadhimisha kwa kuzindua program maalum na kuwapa semina wanawake wa Benki ya hiyo.

Aidha Nsekela alisema mpango huo utakuwa endelevu kwani Benki ya CRDB sio tu kuwa inaamini katika nafasi sawa yaani 50/50, bali imeona ni vema kuwa na mpango maalumu kwa kuwafanya wanawake wawe na wigo mpana zaidi kuweza kupambana kwa kujiamini na kushika nafasi na nyazifa mbalimbali za uongozi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Benki hiyo wakati wa uzinduzi wa program maalumu ya kuwawezesha Wanawake (Mentoring Program for empowering Women) ili waweze kushika nafasi mbalimbali za uongozi, iliyofanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Johari Rotana, jijini Dar es salaam 
Afisa Biashara Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Benki hiyo wakati wa uzinduzi wa program maalumu ya kuwawezesha Wanawake (Mentoring Program for empowering Women) ili waweze kushika nafasi mbalimbali za uongozi, iliyofanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Johari Rotana, jijini Dar es salaam jana.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa (kulia) akizungumza wakati wa mdahalo ulioenda sambamba na uzinduzi wa program maalumu ya kuwawezesha Wanawake (Mentoring Program for empowering Women) ili waweze kushika nafasi mbalimbali za uongozi, iliyofanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Johari Rotana, jijini Dar es salaam jana.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post