Jiji la Arusha nchini Tanzania limeanza operesheni ya kuyafanyia usafi magari ya abiria kwa kuyapulizia dawa ya kuzuia virusi ugonjwa wa corona.
Shughuli ya kuyapulizia dawa imeanza jana Ijumaa Machi 27,2020 na kuongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Fabian Daqarro.
Mhe.Gabriel Daqaro amesema kuwa operesheni hiyo ya upulizaji wa dawa utakuwa endelevu na utashirikisha wadau ambao tayari wameanza kutoa michago yao kuwezesha zoezi hilo.
Aidha Daqarro amewataka wananchi kutokuwa na taharuki na hofu pamoja kuzusha maneno ya upotoshaji juu ya ugonjwa huo bali waachie mamlaka husika kutoa taarifa pamoja na elimu.