ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 154 ZATUMIKA KUJENGA VYUMBA VITATU VYA MADARASA,UKARABATI WA SHULE WILAYANI TANDAHIMBA


 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Sebastian Waryuba akizindua madarasa hayo akiwa na wafadhili waliowezesha mradi huo
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Sebastian Waryuba na Mwenyekiti wa Eclat wakisaini makabidhino hayo
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Sebastian Waryuba akikabidhi hati ya makabidhino Afisa Elimu Msingi Wilaya Hadija Mwinuka
 Matundu ya Choo kwa ajili ya wanafunzi na walimu Wao
Meneja wa mradi Msham Bashir (mzawa qa Luagala)ambaye ndiye aliwashawishi kuja kuboresha miundombinu ya Elimu Wilayani hapo
 Shule ya msingi Luagala 'B' katika muonekano mpya
 Wananchi wa Kijiji Cha Luagala 'B'wakishuhudia uzinduzi wa shule

****
Zaidi ya shilingi Milioni 154 zimetumika kujenga vyumba vitatu vya madarasa na kukarabati shule ya Msingi Luagala 'B' Wilayani Tandahimba

Akizindua madarasa hayo Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Sebastian Waryuba amesema madarasa hayo yamewekwa na madawati tayari kwa wanafunzi kuendelea na masomo

"Tumezindua madarasa haya lakini pia wametukabidhi shule ikiwa katika muonekano unaovutia  ambapo kazi hii imefanywa na taasisi ya Eclat na Upendo ,"amesema Waryuba

Naye Mwenyekiti wa taasisi ya Eclat Toima Kiroya ameeleza kuwa katika mradi huo wameweza kujenga vyumba vitatu vya madarasa,kukarabati majengo 8,kisima chenye ujazo wa Lita 150,000,matundu 16 ya Choo,madawati 65,meza za walimu 16 na viti 16

Hata hivyo Dk Fred Heimbach wa Upendo Society kutoka Ujerumani ameeleza kuwa madhumuni ya ushirika huo ni kuboresha miundo mbinu katika sekta ya elimu

Sambamba na Hilo  Meneja wa mradi huo Msham Bashir ameishukuru serikali kwa kushirikiana  kuanzia ngazi ya Kijiji hadi Wilaya hivyo wananchi wanajukumu lankutunza miundo mbinu hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527