ALIYEWAHI KUWA KATIBU UHAMASISHAJI BAVICHA AJIVUA UANACHAMA WA CHADEMA.......“CHADEMA IMEKUWA KAMPUNI YA MTU BINAFSI NA SIO CHAMA CHA SIASA.”


Aliyewahi kuwa Katibu Mwenezi/ Uhamasishaji  wa Baraza la Vijana la Chama Cha demokrasia na Maendeleo (BAVICHA), Edward Simbeye Leo  February 26, 2020 ametangaza kujivua uanachama wa CHADEMA, kwa kile alichokisema kutokuunga mkono baadhi ya mambo yanayoendelea ndani ya chama hicho cha Chadema na kwamba kwa sasa anatafakari chama gani cha kujiunga.


Sembeye amesema moja ya vitu vinavyokiumiza chama hicho, ni chama  kuendeshwa kwa amri na matakwa ya  Freeman Mbowe ambaye ni  mwenyekiti wa chama hicho na si Katiba ya Chadema.

"Mambo ya Chadema yanatakiwa kuamuliwa kwa mujibu wa Katiba, Kanuni na miongozo ya chama, leo yanaamuliwa kwa kauli na amri za Mbowe, Mwenyekiti ameamua kugeuza chama kuwa mali yake binafsi, lakini tukitoka nje tunawaaminisha umma kuwa chama hichi ni mali ya Watanzania.

Amesema, kutokana na kutokuwa na umoja na msimamo, matokeo yake wamepoteza hata majiji waliyokuwa wakiyaongoza.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post