Angalia picha :WAZIRI KAIRUKI AONGOZA MKUTANO MKUBWA WA MASHAURINO KATI YA SERIKALI,WAFANYABIASHARA NA WAWEKEZAJI MKOA WA SHINYANGA




Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki akizungumza katika mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanyabiashara na Wawekezaji mkoa wa Shinyanga.


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Masuala ya Uwekezaji, Mhe. Angellah Kairuki ameongoza Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ili kusikilizwa na kupata ufumbuzi wa changamoto katika maeneo yao ya uwekezaji na biashara kwa lengo la kuboresha biashara na uwekezaji ili kuongeza wigo wa ajira kwa vijana na kulipa kodi kwa hiari.


Mkutano huo umefanyika leo Jumatano Februari 26,2020 katika Ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na Mawaziri na Manaibu Mawaziri kutoka Wizara nane ikiwemo Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Wizara ya Fedha na Mipango, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Mambo ya Ndani, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Madini. 

Akizungumza katika Mkutano huo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji nchini Mhe.Angellah Kairuki alieleza namna Serikali ilivyoendelea na jitihada za kuhakikisha uboreshwaji wa mazingira ya uwekezaji nchini ikiwa ni pamoja na kutungwa kwa sheria mpya ya uwezeshaji biashara (Business Facilitation Acts).

Mhe. Kairuki alisema uwepo wa mikutano hiyo inaongeza hamasa kwa wafanyabiashara na wawekezaji kueleza kero wanazokabiliana nazo pamoja na kupatiwa majibu ya papo kwa hapo na Mawaziri wa Sekta husika.

“Mikutano imeibua hoja muhimu zilizopatiwa ufumbuzi na mawaziri wa sekta mbalimbali niwatoe shaka Serikali itaendelea kuwaunga mkono na ni vyema mkaendelea kufuata sheria na kanuni zilizopo katika kuwekeza kwenu,”alisisitiza Waziri Kairuki.

Waziri Kairuki aliwataka wafanyabiashara na wawekezaji wanapokuwa na migogoro wasisite kuwasiliana na serikali ili kuitatua na kuepuka kusababisha migogoro kuwa mikubwa.

Alitumia fursa hiyo kuipongeza serikali ya mkoa wa Shinyanga kwa kutenga jumla ya hekta 200 kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vidogo na hekta 640 kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vikubwa katika eneo la Bukondamoyo kata ya Zongomela wilayani Kahama ambalo tayari serikali imetumia shilingi 809,400,000/= kwa ajili ya kuliwekea miundombinu wezeshi ikiwemo barabara,umeme na maji.

"Kuhusu suala la Uwanja wa Ndege wa Ibadakuli nitalifuatilia kwa ukaribu kwani limelalamikiwa kuwa changamoto kwa wafanyabiashara",alisema Kairuki.

Naye Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega aliwahakikishia wafugaji wa samaki kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira bora ya kuwawezesha wafugaji kufuga samaki na kueleza kuwa, mabwawa ya samaki yameongezaka kutokana na jitihada zilizopo na kueleza namna Serikali inavyoendelea kudhibiti uvuvi haramu Baharini na kwenye Maziwa.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashantu Kijaji aliwahakikishia wajumbe wa mkutano huo namna Wizara yake ilivyojipanga kuondoa changamoto za gharama kubwa za mikopo katika benki pamoja na suala la utitiri wa kodi baada ya kulalamikiwa na wafanyabiashala hao.

“Nimewafurahia wana Shinyanga kwa uwazi wenu wa kujieleza vizuri, niwahakikishie kuwa,mwisho wa malalaiko yenu haupo mbali tutahakikisha sekta ya fedha inatatua kero zenu na kushughulikia upatikanaji wa mikopo na kwa gharama zinazoeleweka,”alieleza Dkt. Kijaji.

Kijaji alisema serikali itayafanyia kazi malalamiko ya wafanyabiashara ikiwemo tozo nyingi huku akisisitiza umuhimu wa wafanyabiashara kulipa kodi.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack alisema mkoa wa Shinyanga umefanya jitihada kubwa ya kuvutia Wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ambapo hadi sasa kuna jumla ya Viwanda 729 kati ya hivyo,Viwanda Vikubwa ni 13,viwanda vya kati 11 na viwanda vidogo 705 ambavyo vimeajiri wafanyakazi 10,150. 

Telack alisema mkoa wa Shinyanga umetenga jumla ya hekta 20,289.25 kwa ajili ya uwekezaji kwenye sekta ya biashara,kilimo na viwanda kati ya hekta hizo, Halmashauri ya Mji wa Kahama imetenga hekta 2,000,halmashauri ya Shinyanga 5,560, Ushetu 2,110,Kishapu 10,361.70 na Msalala hekta 257.53. 

Hata hivyo kutokana na ongezeko kubwa la idadi ya watu wanaozaliwa na wanaohamia Telack alisema hali hiyo imesababisha uhitaji wa ujenzi wa shule,vituo vya huduma za afya,ujenzi wa nyumba za kulala wageni na kadhalika. 

“Serikali imetengeneza mazingira wezeshi kwa wazawa kuingia kwenye biashara ya Madini ya almasi kwa kuuelekeza Mgodi wa Almasi wa Mwadui (WDL) kuuza asilimia 5 ya almasi inayozalishwa ndani ya soko la ndani kwa njia ya mnada na uuzaji wa kawaida.Natoa rai kwa wafanyabiashara wote kuchangamkia fursa hii ili baadaye almasi yote inayozalishwa iuzwe ndani ya mkoa wetu na kuongeza ukuaji wa wa uchumi wa mkoa”,alisema Telack.

Kwa Upande wake,Meneja Mahusiano na Maendeleo ya Jamii Mgodi wa Bulyanhulu Dk. Zumbi Musiba akimwakilisha Mkurugenzi wa Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Barrick, alisema Barrick inashukuru kwa fursa ya kufadhili Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ili kushirikiana na serikali kuchangia katika kuendeleza uchumi wa mkoa na nchi kwa ujumla.

"Wengi wa washiriki wa mkutano huo ni wadau wa Kampuni ya Barrick hivyo hiyo ni fursa nzuri ya kusikia wanakabiliwa na changamoto zipi ili kwa pamoja tuweze kuzitafutia ufumbuzi",alisema Dk. Musiba.

Mkutano huo uliohudhuriwa na Wafanyabiashara na Wawekezaji zaidi ya 560 umeandaliwa na Kamati Tendaji ya Baraza la Biashara mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) kwa ufadhili wa Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Dhahabu ya Barrick, Benki ya CRDB,NMB, TPB na NBC. 
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Februari 26,2020 katika ukumbi wa NSSF Mjini Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki akiongoza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Shinyanga Mhe. Zainab Telack akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Shinyanga Mhe. Zainab Telack akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki.
Meneja Mahusiano na Maendeleo ya Jamii Mgodi wa Bulyanhulu  Dk. Zumbi Musiba akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Barrick katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki.
Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Nyabaganga Talaba akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe, Jasinta Mboneko ( wa kwanza kulia) wakiwa ukumbini.
Meza kuu wakifuatilia matukio ukumbini.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Mstaafu Emmanuel Maganga akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki.
Wadau wakiwa katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.
Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Shinyanga Dk. Meshack Kulwa akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki.
Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Mstaafu Emmanuel Maganga. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa.
Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Shinyanga Dk. Meshack Kulwa akiteja jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Shinyanga Mhe. Zainab Telack (kulia).
Naibu Waziri wa  Fedha na Mipango, Dk. Ashantu Kijaji akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.

Naibu Waziri wa  Ujenzi Elias Kwandikwa akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.

Naibu Waziri wa  Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Hamad Masauni akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.
Manaibu Waziri wa Wizara mbalimbali wakiwa ukumbini.

Wadau wakiwa katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.
Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ukiendelea.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mabala Mlolwa akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki.
Mkutano unaendelea.
Naibu Waziri wa  Fedha na Mipango, Dk. Ashantu Kijaji akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constatine  Kanyasu akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki.
Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angellina Mabula akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.
 Wadau wakiwa ukumbini.
Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini Mhe. Jumanne Kishimba akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.
Wadau wakiwa ukumbini.
Mkurugenzi wa Karena Hotel,Josephine Wambura akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.
Mkutano unaendelea.
Mwenyekiti wa Shirikio la Wamiliki wa Shule Binafsi mkoa wa Shinyanga, Jackton Koyi akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.
Wadau wakiwa ukumbini.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kahama Plastic Investment (T) Limited Kazimoto Leonard akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.
Viongozi wa dini wakifuatilia mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.
Mkutano unaendelea.
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.
Meneja wa Benki ya TPB mkoa wa Shinyanga Jumanne Wagana akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.
Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Stanslaus Nyongo akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.
Meneja wa Benki ya NMB Sospeter Magese akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.
Wadau wakiwa ukumbini.
Meneja wa Benki ya NBC mkoa wa Shinyanga Happiness Kizigira akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Saidi Pamui akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.
Wadau wakiwa ukumbini.
Wadau wakiwa ukumbini.
Wadau wakiwa ukumbini.
Mkutano unaendelea.
Mkutano unaendelea.
Mkutano unaendelea.
Wadau wakiwa ukumbini.
Mkutano unaendelea.
Dk. Seif Said kutoka Kahama akizungumza katika mkutano huo.
Mkutano unaendelea.
Mkutano unaendelea.
Mkutano unaendelea.
Katibu wa SHIREMA, Gregory Kibusi akizungumza katika mkutano huo.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga. 
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Nyabaganga Talaba akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.
Mfanyabiashara Edna Catherine Wanna akizungumza katika mkutano huo.
Wadau wakiwa ukumbini.

Awali Mwenyekiti wa Kamati ya amani mkoa wa Shinyanga Sheikh Khamis Balisusa akiomba dua kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini mashariki ya Ziwa Victoria, Dk. Emmanuel Joseph Makala akiomba kabla ya kuanza Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527