Wanaowatoza Wananchi Pesa Ya Nguzo Za Umeme Kukamatwa

Waziri wa Nishati, Dk Merdad Kalemani ameagiza makandarasi au mameneja wanaolazimisha wananchi kulipia nguzo za umeme ili kuunganishiwa nishati hiyo kukamatwa.

Amesema watu hao wanapuuza agizo la Serikali inayotaka nguzo hizo kutolewa bure.

Ametoa ufafanuzi huo Februari 15, 2020 baada ya kupokea malalamiko ya mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Enock Yakobo katika hafla ya ufunguzi wa ofisi ya CCM Mkoa wa Geita.

Yakobo amesema licha ya Serikali kutangaza mara kwa mara kuwa nguzo za umeme ni bure wapo makandarasi wanaoendelea kukaidi agizo hilo na kuwatoza wananchi fedha.

Kalemani amewataka wakuu wa Wilaya kote nchini kusimamia agizo hilo na kuwakamata watakaotoza fedha.

Amebainisha kuwa Serikali inatoa nguzo za umeme bure na wananchi wanapaswa kuchangia Sh27,000 pekee kwa ajili ya kuunganishiwa umeme


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments