WANAFUNZI 14 WAFARIKI KWA KUKANYAGANA KENYA


Wanafunzi 14 wamefariki dunia huku wengine 39 wakijeruhiwa katika Shule ya Msingi Kakamega nchini Kenya kutokana na kukanyagwa na wenzao na kuanguka wakati wakikimbia.

Ajali hiyo imetokea Jumatatu Februari 3 majira ya saa 11 joni wakati watoto hao wakitoka madarasani kurejea makwao, ambapo tayari wanafunzi 20 waliojeruhiwa wameruhusiwa kutoka hospitali.

“Kumpoteza mtoto ni tukio linalouma sana. Natoa salamu za pole kwa wazazi wote waliofiwa na watoto wao,” Waziri wa Elimu, George Magoha amesema.

Kamanda wa Polisi wa Kakamega, David Kabena amesema chanzo cha tukio hilo hakijafahamika lakini amebainisha kuwa tayari uchunguzi umeanza.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post