UPANDE WA MASHITAKA WAOMBA KUKUTANA NA ERICK KABENDERA KWA AJILI YA KUKAMILISHA MAJADILIANO YA KUMALIZA KESI YAKE


Hatima ya kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili, Mwandishi wa Habari, Erick Kabendera itajulikana Februari 17, 2020 baada ya Upande wa Mashtaka kuomba kuzungumza na mwandishi huyo  kwa ajili ya kuingia naye makubaliano.

Hatua hiyo inakuja ni ikiwa ni wiki chache baada ya Kabendera kuomba kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka (DPP) kwa ajili ya maelewano.

Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Janet Mtega kuwa kwa muda mrefu kulikuwa na mchakato wa maelewano baina ya Mshitakiwa na Mkurugenzi wa Mashitaka, hivyo wapo katika hatua ya mwisho.

Amedai kuwa hatua iliyobakiwa ni kuzungumza na mshitakiwa mwenyewe baada ya kuzungumza na mawakili wake, hivyo wanaomba kesi hiyo iahirishwe hadi Jumatatu, Februari 17, 2020.

“Tunawasilisha maombi ya kuzungumza na mshitakiwa kwa sababu tayari tulishazungumza na mawakili wake,”amesema.

Hakimu Mtega amesema kuwa kutokana na ombi hilo la upande wa mashitaka anawakubalia, hivyo anaahirisha kesi hiyo hadi Februari 17, 2020.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post