UPASUAJI WA KUREKEBISHA UKE WAZUA GUMZO...WENGINE WATAKA UPIGWE MARUFUKU

Karibu kliniki 22 za kibinafsi zinatoa huduma ya upasuaji wa kurekebisha uke nchini Ungereza


Wanaharakati wanataka serikali kupiga marufuku upasuaji wa "kurekebishaji uke".

Idadi kubwa ya wanawake Waislamu wako katika harakati ya kutengwa au hata kuuawa katika baadhi ya visa iwapo waume zao au familia watagundua kwamba walishiriki mapenzi kabla ya kuolewa.

Na kutokana na hilo, wengine wao wanaamua kupitia mchakato wa kimatibabu wa kufanyiwa upasuaji ambapo madaktari wanaregesha tabaka la utando kwenye uke.

hata hivyo kuna wasiwasi kwamba marufuku ya kufanya upasuai wa aina hii, kutahatarisha maisha ya wanawake wengi Waislamu na kutafuta huduma hii kinyemela.

Miongozo ya Baraza kuu la Kitiba inasema idhini ya mgonjwa ya kufanyiwa upasuaji huu inastahili kutiliwa shaka iwapo itashukiwa kuwa anahitajika upasuaji kwasababu ya shinikizo fulani ama kwake binafsi au kutoka kwa mtu mwengine.
'kuishi kwa Uwoga'

Halaleh Taheri, mwasisi wa shirika la Wanawake Mashariki ya Kati ameiambia BBC simulizi ya mwanafunzi ambaye ameenda mafichoni mjini London baada ya kuarifiwa kuwa babake amemta mtu kibarua cha kumuua.

Baada ya kwenda Uingereza 2014 kusoma, mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 26, alikutana na mwanamume na kushiriki naye mapenzi.

Lakini babake alipofahamu kuhusu uhusiano wao, alimtaka arejee Morocco na kumpeleka katika hospitali moja ili afanyiwe uchunguzi kama bado ni bikira na matokeo yakaonyesha kuwa tayari amebikiriwa.Mwanamke wa Kiislamu aliyelazimika kufanyiwa upasuaji, wamesema wanaharakati

Alikimbilia Uingereza lakini kwasasa anaishi kwa hofu ya kwamba babake atafahamu kule anakoishi.

Mdogo wa mwalimu mkuu mwenye umri wa miaka 40 mzaliwa wa Morocco, ameiambia BBC kwamba baada ya kulazimishwa kufanyiwa upasuaji wa uke akiwa kwenye miaka ya 20, hangetaka kuona watoto wake wakipitia shinikizo kama hilo na kufanya alichofanya.

"Siwezi kamwe kuwafanyia nilichopita. Najitahidi kuwafunza kuwa huru."

Usiku wa Ndoa

Kwa sasa kuna karibia kliniki 22 za kibinafsi nchini Uingereza zinazotoa huduma ya kurekebisha uke kwa njia ya upasuaji, kulingana na utafiti uliofanywa hivi karibuni na gazeti la Sunday Times.

Kwa wakati huu gharama ya huduma ya upasuaji huo ni hadi £3,000 ambao unachukua karibia saa moja.

Wanaharakati wa maswala ya wanawake, wanasema kuwa kliniki kama hizo zinapata faida sana kutoka kwa wanawake Waislamu ambao wanahofu ya kile kitakachotokea iwapo watagunduliwa kuwa tayari wamebikiriwa usiku wa ndoa yao.

Kuna baadhi ya waathirika ambao wakupitia mtandao wa kliniki moja ya (London's Gynae Centre) wanaarifu kwamba "Baadhi ya ndoa huvunjika" iwapo mume atagundua kwamba mke wake siyo bikra.

Kitengo cha BBC News kimewasiliana na kliniki kupata maoni yao lakini bado hakisema lolote.
'Utamaduni wa Kuogofya'

Waziri wa Afya Matt Hancock alisema kwamba atachunguza namna ya kukamilisha utamaduni huu, lakini Idara ya Afya ikakataa kusema kuhusu vile marufuku hiyo itakavyotekelezwa.

Lakini Miss Taheri akasema: "Wasichana watakufa iwapo marufuku hiyo itafanywa bila mpangilio mzuri."

Dr Khalid Khan, profesa wa masuala ya afya ya wanawake katika Shule ya Tiba ya Chuo Kikuu cha Barts na London, ambaye ameshuhudia upasuaji huu amesema marufuku siyo hatua stahiki ya kuchukuliwa.

Na mradi tu wanaohitaji huduma wanapewa taarifa muhimu, wanawake wanastahili kuachiwa fursa ya kufanya maamuzi ya kile wanachotak.

"Naamini kwamba nia ya madaktari ni ya kuwalinda dhidi ya unyanyasaji," ameongeza.Mfumo wa Infibulation wa kushona sehemu ya uke na kuacha tundu ndogo tu

'Hakuna faida yoyote'

Hata hivyo, Dr Naomi Crouch, mwenyekiti wa Chama cha madaktari wa watoto na vijana Uingereza, ana wasiwasi kuhusu hatua ya wanawake na wasichana kulazimishwa kupitia upasuaji huu ambao haona faida yoyote kiafya.

Anasema kwamba majukumu yake yamewekwa bayana katika miongozo ya Baraza kuu la Kitiba.

"Sisi kama wataalamu wa afya tumefungwa na kiapo tunachokula kudhuru kwa namna yoyote ile wagonjwa."

Colin Melville, mkurugenzi wa kitiba amesema ni muhimu kwa madaktari kutilia maanani kwanza mahitaji na matibabu ya kisaikolojia wanayohitaji waathirika.

"Iwapo mgonjwa anapata shinikizo kutoka kwa wengine la kuchukua hatua kama hii, huenda idhini yao ikawa sio ya kujitolea. Ikiwa daktari atafikia uamuzi kuwa mtoto au kijana kwa hiari yake mwenyewe hangependa kufanyiwa upasuaji huu, basi hakuna budi zaidi ya kuachana na mchakato wote," daktari Melville amesema.
Lakini upasuaji huu unahusu nini na je una faida yoyote?

Aidha upasuaji wa kubadili mdomo wa uke ama uwe mfupi au kubadilishwa umbo kumekuwa maarufu hasa kwa wanawake vijana wa kila asili nchini Uingereza.

Na wanaharakati wanasema, taarifa kuhusu athari za muda mrefu za upasuaji wa aina hizi bado hazifahamiki na wana wasiwasi kwamba wanawake hawapati ushauri mzuri wa kisaikolojia kabla kufanyiwa upasuaji.

Taheri amesema: "Wanawake hawa inafikia wakati wanajikuta wasio na thamani yoyote kama wanadamu zaidi ya kuwa kitu cha kutamaniwa na wengine''.

"Wanawake Waislamu, kinachowasukuma kuchukua hatua ya kufanyiwa upasuaji wa aina hii ni kuziba aibu na hofu ya kuadhibiwa.

"Kwa wengine, ni kutoridhika na jinsi ulivyoumbwa, na fikra za kile ambacho jamii inakuambia ndiyo sawa."
CHANZO - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post