DC MJEMA AWAPONGEZA VIONGOZI WA DINI WANAOLIOMBEA TAIFA KWA NIA NJEMA


 Na Azmala said - Dar es salaam

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema amewapongeza viongozi wa madhehebu ya dini wanaoliombea taifa kwa nia njema bila uchochezi wa kidini.
Akizungumza katika Kanisa la Amani Christian  Center  lililopo Liwiti Mtaa wa Amana jijini Dar es salaam amewataka viongozi wa dini na waumini wafanye mambo mema kwa moyo wote kama walivyojitolea katika kuliombea taifa,viongozi na kipindi hichi cha uchaguzi 2020.

Mjema amesema yeye kama kiongozi wa serikali na msaidizi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amelipongeza na kulishukuru kanisa hilo kwa kujitolea kwa maombi tangu Januari 2 hadi 31kwa kuliombea taifa. 

Mjema amesema serikali ya awamu ya tano katika kuhakikisha inasaidia wananchi katika kujiondoa katika umasikini na kufikia katika uchumi wa viwanda wa kati ,Rais John Pombe Magufuli aliagiza manispaa zote zitenge asilimia 10 za mikopo asilimia nne kwa akina mama na nne vijana na mbili ni watu wenye ulemavu na haina riba hivyo ni vyema wananchi wachangamkie fulsa hiyo ya mikopo bila riba.

Aidha Mkuu wa wilaya amempongeza askofu Lawrence Kameta na kusema dini zote ni sawa na wote wawe na amani akisema "Amani ni neno dogo lakini lina maana kubwa".

Kwa upande wa Baba Askofu Kameta amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa ujio wake na kumwambia aendelee kushirikiana kwa moyo wote bila ubaguzi wowote.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post