MSANII MAARUFU WA NYIMBO ZA INJILI, KIZITO MIHIGO AJINYONGA KITUO CHA POLISI


Mwanamuziki maarufu kwa nyimbo za injili nchini Rwanda Kizito Mihigo.

Polisi ya Rwanda imetangaza kwamba msanii maarufu wa nyimbo za injili, Kizito Mihigo ''amejinyonga'' Polisi wa Rwanda wanasema.

Kwa mujibu wa tangazo la polisi, maiti ya msanii huyo imepatikana katika chumba alimokuwa anazuiliwa kwenye kituo cha polisi mtaa wa Remera, mjini Kigali.

Polisi imesema kwamba amejinyonga siku tatu baada ya kukamatwa karibu na mpaka baina ya Rwanda na Burundi katika kile ambacho polisi ilisema alikuwa na nia ya kutoroka nchi na kujiunga na makundi ya waasi dhidi ya Rwanda.

Wachunguzi nchini Rwanda wanasema kwamba uchunguzi kuhusu kifo chake umeanzishwa . Polisi wanasema kwamba Mihigo alijitoa uhai katika kisa kilichowashangaza mashabiki wake wengi na raia wa Rwanda.

''Uchunguzi umanzishwa . mwili wake umepelekwa katika chumba cha karibu cha kuhifadhi maiti ambapo uchunguzi katika mwili wake utafanywa . Alikuwa akizuilia pekee katika kituo cha wachunguzi cha Rwanda katika eneo la Remera mji mkuu wa Kigali ambapo alipatikana amejinyonga ndani ya seli yake mapema alfajiri. Alitumia nguo aliokuwa anatumia kulalia kujinyonga.

Hatahivyo wanaharakati wanaoishi ughaibuni wamepinga taarifa iliotolewa na polisi hao.

Wamesema kwamba mwanamuziki huyo hakutaka kujiunga na kundi la waasi nchini Burundi na kwamba alitaka kwenda Ubelgiji ambapo alikuwa akiishi .

Pia wanaamini kwamba hakujiua katika kituo cha polisi alipokuwa anazuiliwa na kwamba huenda aliuawa.

Muziki wa kizito ndio chanzo cha matatizo yaliomkumba . Katika wimbo mmoja alipendekeza kwamba kila mtu aliyeuawa katika mauaji ya kimbari ya 1994 anapaswa kukumbwa awe Mtutsi ama Muhutu.

Wanasema kwamba mamlaka imeliona hilo kama changamoto ya wazi dhidi yake na kwamba mauaji hayo yalitekelezwa na Watutsi.

Wakosoaji wa serikali wanaamnini kwamba kutokana na hilo Kizito alilengwa.

Mwanamuziki huyo alikua ameanza kuchunguzwa kuhusiana na madai hayo pamoja na kutaka kuwahonga wananchi waliomkataa.

Mwaka uliopita aliachiwa huru kwa msamaha wa rais baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 10 jela kwa hatia ya kutaka kumuua rais na kuhamasisha raia kupinga serikali.Mwaka 2015, Bwana Kizito alikutwa na hatia kwa kosa la jaribio la kutaka kumuua Rais Paul Kagame na kuhamasisha vurugu dhidi ya serikali na kufungwa lakini baadae alisamehewa

Kumekuwa na hisia mseto katika mitandao ya kijamii kuhusiana na kifo cha ghafla cha msanii huyo wa muziki wa injili huku baadhi ya watu wakitaka majibu kutoka kwa serikali.

Kizito, aliyekuwa na miaka 38 alipata umaarufu kutokana na nyiimbo zake kama vile 'Inuma' unaomaanisha njiwa na 'Igisobanuri cy'urupfu' ambao unaelezea kifo ni nini.
Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527