SERIKALI YA TANZANIA YAMUONYA NABII ANAYEJITANGAZA ANA UWEZO WA KUTIBU CORONA | MALUNDE 1 BLOG

Friday, February 14, 2020

SERIKALI YA TANZANIA YAMUONYA NABII ANAYEJITANGAZA ANA UWEZO WA KUTIBU CORONA

  Malunde       Friday, February 14, 2020
 Na Ahmed Mahmoud,Arusha

Serikali ya Tanzania imemuonya vikali mtu anayejiita Nabii Namba saba ambaye jina lake halisi ni Mosses Mollel kuwa itamchukulia hatua kali iwapo atashindwa kuthibitisha madai  kuwa na uwezo wa kutibu virusi Vya ugonjwa wa Corona.

Nabii huyo ambaye taarifa zake zilianza kusambaa mwishoni mwa wiki iliyopita kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii akidai anayo dawa ya kutibu ugonjwa hatari wa Corona ulioanzia nchini China na kusababisha Vifo Vya watu zaidi ya 1100 hadi sasa,ametakiwa kujisalimisha wizara ya afya na kuthibitisha taarifa hizo. 


Akiongea na Vyombo Vya Habari jijini Arusha,Naibu Waziri wa Afya,Dkt Faustine Ndugulile ameeleza kuwa anazo taarifa za Nabii huyo kujitangaza kuwa anayodawa ya kutibu ugonjwa huo na kumtaka athibitishe kauli yake


“Kimsingi nimeiona hiyo taarifa ya huyo mtu  anayejiita Nabii Saba kuwa anayo dawa ya kutibu ugonjwa wa Corona ,ila hapa kwetu Tanzania hatuna maambukizi yoyote ya ugonjwa huyo ,tunachotaka huyo mtu  atuthibitishie uwezo wake wa kutibu huyo ugonjwa wa Corona” Amesema Ndugulile


Ameongeza kuwa iwapo atashindwa kuthibitisha atachukuliwa hatua Kali za kisheria.


Amesema hadi sasa Serikali imetuma wataalamu wake kwenda kumsaka na kumhoji kama anavyo vibali Vya kutoa huduma ya Tiba na kujitangaza kuwa anatoa Huduma ya kutibu ugonjwa huo  hatari ambao hadi sasa mataifa bado yanahaha kusaka  Tiba ya ugonjwa huo.


Nabii Namba Saba ambaye ni mkazi wa Ngaramtoni Wilayani Arumeru,Mkoani Arusha amekuwa akijitangaza kuwa anayo dawa ya kutibu ugonjwa huo wa corona na kuweka mawasiliano yake  kwenye mitandao .


“Ninayodawa hapa Arusha ya kutibu virusi Vya Corona inayowaua Wachina na mataifa mengine. ” sauti ya Nabii huyo.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post