MBATIA AISHAURI SERIKALI KUHUSU MASUALA YA MAJANGA YANAYOTOKEA NCHINI | MALUNDE 1 BLOG

Friday, February 14, 2020

MBATIA AISHAURI SERIKALI KUHUSU MASUALA YA MAJANGA YANAYOTOKEA NCHINI

  Malunde       Friday, February 14, 2020

Mwenyekiti Taifa wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, ameishauri Serikali kuweka taasisi au mamlaka ya kuweza kusimamia kwa ukaribu masuala ya majanga yanayotokea nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mbatia aliyataja majanga hayo kuwa ni pamoja na mvua zilizosababisha mafuriko na watu kadhaa kupoteza maisha.

Aidha alisema sheria ya mwaka 2015 walishauri kuwepo na mamlaka kamili ya kukabiliana na majanga hayo na inatakiwa kusema ni lazima isimamie majanga yote na iwe inachukua hatua haraka.

Mbatia ambaye pia ni Mbunge wa Vunjo, alisema kuwa suala la maafa ni suala la kitaalamu, hivyo mamlaka hiyo ikiundwa inakuwa na wataalamu maalumu ambao watakuwa maalum kwa kusimamia majanga hayo.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post