MAMA SALMA KIKWETE AWAOMBA VIONGOZI WA DINI KUHIMIZA WAUMINI KUPIMA VVU

Mbunge wa kuteuliwa na Mhe. Rais lakini pia ni Mke wa Rais Mstaafu  Mama Salma Kikwete leo amekuwa mgeni rasmi akimuwakilisha Spika wa Bunge la Tanzania kwenye mkutano wa taasisi na viongozi wa dini katika kuyafikia malengo ya 95 95 95  uliofanyika katika Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.


Mkutano huu umeshirikisha viongozi wakuu wa dini kutoka BAKWATA, CCT, CPCT, TEC, SDA na wadau wengine wakiwemo wajumbe kutoka Kamati ya Bunge ya kudumu ya UKIMWI, Kifua Kikuu na dawa za kulevya na TACAIDS na Viongozi wa Dini pamoja Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ukimwi. Lengo kuu likiwa ni wananchi kujitokeza kupima Virusi vya Ukimwi nchini ili kuweza kujua Afya zao

Akizungumza katika Mkutano huu  umefanyika katika Ukumbi wa Hotel ya Mount Meru Jijini Arusha Mhe Salma Kikwete alisema"Wote kwa pamoja tuwe na moyo wa kuondoa Unyanyapaa na Ubaguzi kwa watu wenye Ukimwi Tanzania na badala yake tuwajali na tuwapende sisi sote ni waja wa Mwenyezi Mungu".

Pia Mama Salma Kikwete amewaomba viongozi wa dini Tanzania pindi watowapo neno kwa waumini wao basi wasikose kuwahimiza kwenda kupima na kujua Afya zao maana kwa sasa Tanzania tuna kauli moja tu “Tanzania bila Ukimwi inawezekana”.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post