Picha : WAKENYA WAJITOKEZA KUUAGA MWILI WA RAIS MSTAAFU WA KENYA DANIEL ARAP MOI


Mwili wa rais mstaafu wa Kenya Daniel Toroitich Arap Moi ukiwasili katika bunge kutoka chumba cha kuhifadhi maiti cha Lee Funeral jijini Nairobi mapema leo.
Rais mstaafu Daniel Toroitich Moi
Mwili wa rais mstaafu wa Kenya Daniel Toroitich Arap Moi umewasili katika bunge kutoka chumba cha kuhifadhi maiti cha Lee Funeral jijini Nairobi mapema leo.

Wakenya kutoka matabaka mbalimbali tayari wameanza kuutazama mwili huo wa kiongozi huyo wa zamani .


Onyo: Baadhi ya wasomaji wanaweza kufadhaishwa na picha hizi

Hatua hiyo inajiri baada ya rais Uhuru Kenyatta aliewasili kutoka nchini Marekani mapema leo kuwa mtu wa kwanza kuutazama mwili huo.Rais Uhuru Kenyatta na mkuu wa majeshi Meja jenerali Samuel Mwathethe

Uhuru alipokewa na naibu wake wa rais William Ruto na mkuu wa majeshi Samson Mwathethe huku usalama ukiimarishwa.

Ruto aliwasili katika majengo ya bunge mwendo wa saa tatu na dakika 50 akiandamana na maafisa wa serikali.

Msafara wa gari lililokuwa likiusafirisha mwili huo kutoka chumba cha Lee ulipitia barabara ya alley Road na kuingia Kenyatta Avenue kabla ya kuingia katika barabara ya bunge ambapo gwaride la kijeshi lilifanywa kutoa heshima.

Moi ambaye aliaga dunia siku ya Jumanne akiwa na umri wa miaka 95 atazikwa nyumbani kwake huko kabarak katika kaunti ya Nakuru tarehe 12 mwezi Februari.Wakati rais Uhuru Kenyatta alipowasili katika majengo ya bunge kutoa heshima zake za mwisho kwa marehemu rais Mstaafu Daniel Moi

Serikali ilitangaza siku ya Jumanne tarehe 11 mwezi Februari kuwa siku kuu kwa raia kushiriki katika ibada ya mazishi ya mwili wa kiongozi huyo wa zamani.
Wakenya walipanga milolongo mirefu ili kutoa heshima yao ya mwisho kwa rais mstaafu

Kwa sasa wananchi waliopanga milolongo mirefu wamepewa fursa kuutaza mwili huo .Shuguli ya kuutazama mwili huo itafanyika kwa siku tatu hadi lkufikia Jumatatu.Wakenya waliojitokeza katika maeneo ya bunge la Kenya ili kutoa heshima zao za mwisho kwa rais mstaafu Daniel arap MoiWakenya wakizidi kumiminika ndani ya majengo ya bunge ili kutoa heshima kwa zao za mwisho kwa rais mstaafu Daniel Moi

Tangazo kutoka Ikulu lilisema kuwa mzee Moi, hata baada ya kuondoka madarakani aliendelea kulitumikia taifa la Kenya na Afrika kwa kuwafundisha viongozi wa Kenya na nje ya Kenya, akiendelea kushiriki kwenye maendeleo ya miradi mbalimbali na kazi za misaada akiihubiri amani, upendo na umoja barani Afrika na duniani.

Mzee Moi aliiongoza Kenya kuelekea kurudisha mfumo wa vyama vingi na katika vipindi vingine vingi vya changamoto; na kumalizika kwa mchakato wa kukabidhi madaraka kwa amani mwezi Desemba mwaka 2002, wakati huo mchakato ambao ulikuwa nadra kufanyika Afrika, ambao uliweka mfano barani afrika na nje ya bara tangu wakati huo.
Daniel Arap Moi: Maisha yake ya siasa na mitazamo kinzani

''Hiba yake inaishi Kenya hata leo. Filosofia ya Nyayo kuhusu 'amani, upendo na umoja' ilikuwa wimbo wake kipindi chake kama kiongozi wa nchi na serikali''. Ilieleza taarifa ya Ikulu.
CHANZO - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post