MGANGA WA KIENYEJI ALIYESABABISHA WANAWAKE 29 WABAKWE NA KUUAWA ATIWA MBARONI

Mganga wa kienyeji anayedaiwa kusababisha wanawake 29 kubakwa na kisha kuuawa baada ya kutoa masharti ya dawa kwa mtu aliyekua akitaka utajiri, amekamatwa na Polisi waliofanya oparesheni ya siku 11 maeneo ya Kanda ya Ziwa.

Mbali na mganga huyo, pia Polisi wanaishikilia fimbo ya mganga mmoja wa kienyeji iliyotumika kuwaaminisha wakata mapanga walioua askari wawili wa kituo cha polisi Nguruka mkoa wa Kigoma, askari mmoja wa Suma JKT na mgambo wa Mkoa wa Tabora, kisha kutolewa sehemu zao za siri kwa ajili ya dawa.


Akizungumza na waandishi wa habari  wakati akitoa tathmini ya opareshini maalumu ya kudhibiti matukio ya mauaji ya kupiga ramli chonganishi na makosa mengine kwa mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza na Shinyanga, Mkuu wa operesheni maalumu wa jeshi la Polisi, Mihayo Nsekela leo Ijumaa Februari 14, 2020,  amesema inadaiwa fimbo hiyo ilitumika kuwakinga wakata mapanga na nguvu ya sheria pindi wanapokwenda kwenye matukio ya kihalifu ili wasikamatwe.

Katika operesheni , wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wa mauaji hayo ambao wapo wakata mapanga 44, watuhumiwa wa ramli chonganishi 75, kufanya uganga bila kibali, unyang’anyi wa kutumia silaha, kupatikana na nyara za Serikali, wizi wa mifugo na watuhumiwa wa makosa mengine.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post