MBUNGE WA VITI MAALUM (CHADEMA) ALILIA NYONGEZA YA MISHAHARA KWA WAFANYAKAZI


Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Ruth Mollel ameishauri Serikali  kuweka nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa Serikali kwa sababu wana hali mbaya.

Ruth ametoa kauli hiyo leo Jumanne Februari 4, 2020 wakati akichangia taarifa tatu za utekelezaji wa shughuli za kamati za Utawala na Serikali za Mitaa, Katiba na Sheria pamoja na Sheria Ndogo.

Ruth amesema katika taarifa zote alizosoma hakuna sehemu wamezungumzia kundi kubwa la watumishi wa umma ambalo ni raslimali watu.

Amesema kwa muda wa miaka minne hawajawahi kuongezewa mishahara na kwamba hilo jambo amekuwa akilisema mara nyingi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post