MBUNGE APELEKA NZIGE BUNGENI


Video ya mbunge mmoja wa Uganda aliyebeba na kupeleka nzige bungeni imesambazwa katika mitandao ya kijamii.

David Obala ambaye anaiwakilisha kaunti ya Ngora Mashariki mwa Uganda , aliwapeleka nzige hao bungeni siku ya Jumanne ili kupinga hatua ya serikali ya kuchelewa kuliangazia janga la kukabiliana na mlipuko wa wadudu hao ambao wameharibu mimea katika eneo la Afrika mashariki hatua inayozua hofu ya kusababisha baa la njaa.

Baada ya mbunge mwIngine kulalamika, bwana Obala alilazimika kuikabidhi chupa iliojaa nzige kwa afisa wa bunge anayesaidia katika kuweka amani bungeni.

Spika alitaka kuelezewa kila wiki kutoka kwa wizara kuhusu hatua ya serikali ya kuwanyunyuzia dawa wadudu hao.

Gazeti la Daily Monitor nchini Uganda lilituma ujumbe wa twitter wa video hiyo ambapo mbunge huyo alionekana akiwabeba nzige hao.


Kulingana na Daily Monitor, tayari serikali imenunua lita 10,000 ya dawa ya wadudu hao ambayo hutumika kote duniani kwa unyunyizaji wa angani.

Dawa hiyo inatarajiwa kuwasili nchini humo siku ya Ijumaa kutoka nchini japan , kulingana na maafia katika wizaRa ya kilimo.

Wadudu hao wamedaiwa kusambaa katika wilaya 17 nchini Uganda ikiwemo Acholi, karamoja, Teso na maeneo yaliopo Magharibi mwa mto Nile.
Wilaya hizo ni Abim, Kaabong, Nakapiripirit, Amudat, Agago, Katakwi, Nabilatuk, Moroto, Kitgun, Soroti na Kole miongoni mwa maeneo mengine.
Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post