MBUNGE CHADEMA CECIL MWAMBE, AJIUZULU NA KUJIUNGA CCM

Mbunge wa Ndanda Mkoani Mtwara (CHADEMA), Cecil Mwambe  amejiuzulu nafasi hiyo na kutangaza kuhamia CCM.


Mwambe amechukua uamuzi huo leo Februari 15, 2020 katika makao makuu ya CCM Lumumba, jijini Dar es salaam

Takribani miezi  miwili iliyopita, Mwambe  alijitosa kugombea uenyekiti wa Chadema akichuana na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe

Akizungumza kuhusu uamuzi wake huo Mwambe amesema vyama vya upinzani nchini vina safari ndefu ya kujenga demokrasia ya kweli, hivyo ameona  atakuwa anajidanganya na kuwadanganya wapiga kura wake kubaki katika vyama vya namna hiyo wakati bado anatamani kuwatumikia wananchi wa Ndanda.

Mwambe  alijiunga  Chadema mwaka 2015 akitokea CCM ambako jina lake lilikatwa katika mchakato wa kura ya maoni kuwania kupitishwa kugombea ubunge


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post