MBOWE AMWANDIKIA BARUA RAIS MAGUFULI


Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe amemwandikia barua Rais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli ili kumuomba alete utengamano wa kitaifa.

Akizungumza Makao Makuu ya Chadema Jijini Dar es Salaam leo,  Mbowe amesema kwa hali ilivyo sasa ikiwemo baadhi ya mataifa kuanza kuitenga Tanzania ni vema kukawa na maridhiano yatakayolifanya taifa hili kuwa lenye umoja na mshikamano.

Akifafanua Mwenyekiti huyo amesema, kuna ulazima Rais akaunda tume ya maridhiano ili kuepusha malalamiko kutoka kwa wananchi


Kuhusu uchaguzi wa Serikali za mitaa, Mbowe ametaka ufutwe na urudiwe.

"Kufutwa kwa uchaguzi huu kutahalalisha kuwa uchaguzi wa mwaka huu (uchaguzi mkuu) utakuwa huru na wa haki. Uchaguzi huu ukafanyike sambamba na uchaguzi wa madiwani, wabunge na Rais.” amesema Mbowe.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post