ALIYEKUWA KATIBU MKUU WA CHADEMA DK. VICENT MASHINJI AHAMIA CCMAliyekuwa katibu mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji amejiunga na CCM leo Jumanne Februari 18, 2020 na kupokelewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM nchini Tanzania, Humphrey Polepole katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es salaam.

Dk Mashinji amejiunga CCM ikiwa imepita miezi miwili tangu ufanyike mkutano mkuu wa Chadema na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kutompendekeza tena kuwa katibu mkuu.

Badala yake, Mbowe alimpendekeza mbunge wa Kibamba, John Mnyika kuwa katibu mkuu wa tano wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini Tanzania, kupigiwa kura na baraza kuu.

Baada ya kukosa nafasi hiyo, Dk Mashinji alieleza masikitiko yake kwamba alitamani kuendelea kuwa katibu mkuu ili aweze kumalizia mipango aliyokuwa nayo, ikiwemo maandalizi ya uchaguzi mkuu wa Oktoba, 2020.

Katika maelezo yake ya leo, Dk Mashinji amesema, “nimuombe mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli kama ataridhia anipe nafasi ya kujiunga na CCM ili niweze kuchangia maendeleo ya nchi yangu.”

Amesema CCM ina nia ya kuwapa wananchi maendeleo tofauti na chama alichotoka, “ninaona kabisa CCM kiko tayari kuwaendeleza Watanzania na kule nilikotoka huo utayari siuoni.”

Baada ya kueleza hayo, Polepole alimkaribisha,“mimi nikuhakikishie kwa niaba ya wakuu wa chama wakiongozwa na ndugu Magufuli nimekupokea rasmi karibu sana CCM.”

Dk Mashinji ni nani?


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post