LUKUVI ATIMIZA AGIZO LA RAIS MAGUFULI ...AKABIDHI EKARI 715 ZA ARDHI KWA MANISPAA YA KIGAMBONI


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi  William Lukuvi amekabidhi ekari 715 za ardhi kwa manispaa ya Kigamboni kama alivyoagizwa na Rais John Magufuli wiki iliyopita.

Februari 11, 2020 wakati akizindua ofisi za mkurugenzi na mkuu wa wilaya ya Kigamboni pamoja na hospitali ya wilaya hiyo, Rais Magufuli alimwagiza Lukuvi kuhamisha umiliki wa ekari hizo kutoka katika wizara yake kwenda kwa manispaa hiyo.

Leo Jumatatu Februari 17, 2020 , Lukuvi akiambatana na katibu mkuu wa wizara hiyo, Mary Makondo wamekabidhi ekari hizo kwa viongozi wa wilaya na manispaa ya Kigamboni akiwamo mkuu wa wilaya hiyo, Sarah Msafiri.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527