LUKUVI AMSIMAMISHA KAZI OFISA ARDHI ALIYETAJWA NA RAIS MAGUFULI | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, February 18, 2020

LUKUVI AMSIMAMISHA KAZI OFISA ARDHI ALIYETAJWA NA RAIS MAGUFULI

  Malunde       Tuesday, February 18, 2020

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , William Lukuvi amemsimamisha kazi ofisa ardhi wa Wilaya ya Kigamboni ambaye siku kadhaa zilizopita Rais Magufuli alitaka achukuliwe hatua kwa kuwa ni mtoro.

Siku hiyo Magufuli alisema, “Nina tatizo na ofisa ardhi wa Kigamboni ni mtoro na hajafanya kazi karibu miezi mitatu, aliandikiwa barua na Wizara ya Ardhi ili ashughulikiwe ila bado wizara wanaleta mshahara wake. Najua wizara watafikishiwa ujumbe, kama ni mtoro atoroke kabisa, sifahamu mkurugenzi mmechukua hatua gani kwa ofisa ardhi huyo ambaye hafanyi kazi.”

Katika maelezo yake ya jana wakati akikabidhi ekari 715 za ardhi kwa manispaa ya Kigamboni kama alivyoagizwa na Rais Magufuli, Lukuvi alisema mtumishi huyo amesimamishwa kazi.

"Bahati nzuri  tulishapata barua kutoka kwa mkurugenzi wa Kigamboni na tumeshamsimamisha kazi wakati hatua za kinidhamu zikiendelea .Kama kutakuwa na uhitaji tutaleta mtu mwingine," alisema Lukuvi.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post