KESI YA KABENDERA KUENDELEA TENA LEO | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, February 11, 2020

KESI YA KABENDERA KUENDELEA TENA LEO

  Malunde       Tuesday, February 11, 2020

Leo Februari 11, 2020, Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwandishi wa Habari, Erick Kabendera, itatajwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam.

Kesi hiyo ilikuwa inatajwa jana katika Mahakama ya Hàkimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Janeth Mtega na kuahirishwa hadi leo.

Wakili wa Serikali, Faraji Nguka akiiwakilisha Jamhuri, alidai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, akaomba iahirishwe hadi leo.

Januari 27, mwaka huu wakati kesi hiyo inatajwa, upande wa Jamhuri ulidai majadiliano na Mkurugenzi wa Mashtaka  nchini (DPP) ya jinsi ya kumaliza kesi hiyo yanaendelea.

Kabendera anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka matatu likiwamo la utakatishaji wa zaidi ya Sh milioni 173.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post