KABENDERA KUENDELEA KUSOTA RUMANDE.....NI BAADA YA HAKIMU KUPATA UDHURU LEO


Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mwandishi wa habari, Erick Kabendera imekwama kuendelea katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya hakimu anayeisikiliza, Janeth Mtega kupata udhuru.

Kwa mujibu wa ratiba ya kesi hiyo leo ilitegemewa kuwa ni hatma ya mwisho ya Kabendera kusota rumande tangu alipopandishwa kizimbani Agosti 5,mwaka  2019 baada ya kuingia makubaliano na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP).

Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon  amedai mbele ya Hakimu Mkazi Vicky  Mwaikambo kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kutajwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Janet Mtega anayesikiliza kesi hiyo hayupo hivyo ameomba kesi hiyo iahirishwe hadi tarehe nyingine.Hakimu Mwaikambo ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 24, 2020 kwa ajili ya kutajwa.

Katika kesi hiyo, Kabendera anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji wa Sh.Mil 173.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post