JESHI LA POLISI DODOMA LAMUITA MWANAHARAKATI CYPRIAN MUSIBA KWA MAHOJIANO KUHUSU TUHUMA ZA KUTAKA KUUAWA

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Jeshi la Polisi mkoani Dodoma limemuita kwa mahojiano mwanaharakati huru Cyprian Musiba  baada ya kutoa tuhuma mbalimbali za kutishiwa kuuawa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Februari 24,2020 jijini Dodoma Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto amesema Musiba kupitia baadhi ya magazeti hapa nchini amechapisha taarifa za kulalamika kutishiwa kuuawa  na baadhi ya wanasiasa .

Hivyo Kamanda Muroto ametoa Rai  kwa wananchi kuacha tabia ya kutoa habari za makosa ya jinai kwenye vyombo vya habari bila kujulisha vyombo vya dola na jeshi hilo limemuita  Musiba kwa Mahojiano zaidi dhidi ya Malalamiko yake.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post