JAMII YATAKIWA KUTUMIA FURSA YA KILIMO ILI KUJIKWAMUA KIMAENDELEO

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Jamii imetakiwa kutumia fursa ya kilimo kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi kuondokana na upungufu wa chakula katika maeneo mbalimbali nchini kwa kutumia fursa ya mvua zinazoendelea kunyesha badala ya kulalamika kuwa maisha ni magumu.

Hayo yamesemwa na mtaalamu wa masuala ya kilimo AMBAYE kwa sasa anajishughulisha na uzalishaji wa mbegu za mazao mbalimbali  ikiwemo karanga na mtama jijini Dodoma 

ITHAN CHAULA amesema kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakitafsiri kilimo kama shughuli ambayo hufanywa na watu wa vijijini akiongeza kuwa sekta hiyo inapaswa kuheshimiwa, kuboreshwa kutoka kilimo cha jembe la mkono na kuwa kilimo cha kisasa.

Amebainisha kuwa  bado wakulima wanahitaji elimu  ya kilimo salama kukabiliana na changamoto ambazo hujitokeza  kama vile sumukuvu wakati wa kupanda, kuvuna na kuhifadhi akiomba serikali kupitia maafisa ugani kutembelea wakulima hasa maeneo ya vijijini kuwapa elimu na mbinu za kilimo bora chenye tija kuachana   na kilimo cha mazoea.

Chaula amewahimiza wakulima hasa mkoa wa dodoma kutumia vizuri utabiri wa hali ya hewa  ambao umekuwa ukitolewa kupanda mazao ambayo yanaweza kuhimili kujipatia chakula na kuyauza kujipatia kipato.

Aidha amepongeza serikali kwa juhudi inazofanya kuhakikisha mkulima anapatiwa mbegu akiiomba kurahisisha mchakato wa upatikanaji wa mbegu hizo  kwa bei rafiki na kwa wakati kumuwezesha mkulima kuendana na msimu
husika.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527