Picha : KAMPUNI YA JAMBO YAMWAGA MSAADA KITUO CHA WATOTO WENYE UALBINO BUHANGIJA


Kampuni ya vinywaji Jambo Products ya mkoani Shinyanga, imetoa misaada mbalimbali ikiwemo chakula kwenye kituo cha kulea watoto wenye ualbino cha Buhangija Jumuishi kilichopo Mjini Shinyanga 

Akizungumza wakati wa kutoa msaada huo leo Alhamis  Februari 20,2020, Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Esme Salum, akiambatana na wachezaji wa timu ya Stand United ambayo wanaifadhili, amesema wameamua kutoa sehemu ya faida ambayo wanaipata kusaidia watoto hao wenye ualbino ili kuwapa faraja.

Amesema watoto hao wenye ualbino wanapaswa kutembelewa na kupewa misaada ya vitu mbalimbali ikiwamo chakula, ili wapate faraja na kujiona jamii ipo pamoja nao na haijawatenga kwani wao ni watu kama wengine.

“Sisi kampuni ya Jambo tumeambatana na wachezaji wa timu ya Standi United ya hapa Shinyanga mjini ambayo tunaifadhili, kuja kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto hawa wenye ualbino, ikiwemo unga wa ngano, chumvi, sabuni za kufulia, mafuta ya kujipata pamoja na juisi,”amesema Salum.

“Zoezi hili la kuja hapa kwenye kituo hiki cha watoto wenye ualbino litakuwa endelevu kwa sababu bado wanahitaji msaada wetu wa kutatua baadhi ya changamoto ambazo zinawakabili ili wapate kuishi kwa furaha,”ameongeza.

Nao baadhi ya watoto hao akiwemo Simon Paulo, wameishukuru kampuni hiyo ya Jambo kwa kutoa msaada huo wa chakula pamoja na vitu vingine, huku wakitoa wito kwa wadau wengine wa maendeleo wajitokeze kuwasaidia, kwani bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo vifaa vya michezo.

Kwa upande wake Msimamizi Mkuu wa kituo hicho mwalimu Selemani Kipanya, amesema wanafarijika sana kwa kupewa msaada huo ikiwamo chakula, na kubainisha jumla ya watoto wanaohifadhiwa kwenye kituo hapo wapo 228, wasioona 23, viziwi 74 pamoja na wenye ualbino 131.


TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Mkurugenzi wa kampuni ya vinywaji ya Jambo Esme Salum, akizungumza kwenye kituo cha watoto wenye ualbino cha Buhanghja Shinyanga mjini wakati alipofika kutoa msaada leo Februari 20,2020. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog

Meneja Rasilimali watu kutoka Kampuni ya Jambo Happy Elly Sopillan, akizungumza kwenye kituo hicho cha watoto wenye ualbino.

Kiongozi wa timu ya Stand United Msenda Msenda akizungumza kwenye kituo hicho cha kulea watoto wenye ualbino cha Buhangija.

Meneja wa timu ya Stand United Fred Masai, akizungumza kwenye kituo hicho cha kulea watoto wenye ualbino cha Buhangija.

Msani wa uchekeshaji kutoka kikundi cha Futuhi Andrew Ngonyani maarufu Brother K, akizungumza kwenye kituo hicho cha watoto wenye ualbino Buhangija na kuipongeza kampuni ya Jambo kwa kutoa msaada kwa watoto hao.

Brother K, akizungumza na watoto wenye ualbino kwenye kituo cha Buhangija.

Mwalimu Selemani Kipanya ambaye ni mlezi mkuu wa kituo hicho cha kulea watoto wenye ualbino cha Buhangija, akizungumza wakati wa kuwakaribisha wageni kutoka kampuni ya vinywaji ya Jambo kwa ajili ya kutoa msaada wa vitu mbalimbali.

Mkurugenzi wa kampuni ya vinywaji ya Jambo Esme Salum akikabidhi msaada kwa watoto wenye ualbino.

Mfanyakazi wa kampuni ya vinywaji ya Jambo Hamduni Nassor akiwa amebeba unga kwa ajili ya kuwakabidhi watoto wenye ualbino wanaolelewa kwenye kituo cha Buhangija Shinyanga mjini.

Mkurugenzi wa Kampuni ya vinywaji ya Jambo Esme Salum, akigawa juisi kwa watoto wenye ualbino.

Mkurugenzi wa Kampuni ya vinywaji ya Jambo Esme Salum, akigawa juisi kwa watoto wenye ualbino.

Baadhi ya wachezaji wa timu ya Stand United wakigawa juice kwa watoto wenye ualbino.

Brothe K akigawa juisi kwa watoto wenye ualbino.

Watoto wenye ualbino wakiwa na juice kutoka kampuni ya vinywaji ya Jambo.

Bidhaa ambazo zimegawiwa kwa watoto wenye ualbino.

Bidhaa ambazo zimegawiwa kwa watoto wenye ualbino.

Baadhi ya wachezaji wa timu ya stand united wakiwa kwenye kituo cha kulea watoto wenye ualbino cha Buhangija.

Mtoto mwenye ualbino Simon Paulo akitoa shukrani ya msaada huo kwa niaba ya wenzake.

Mkurugenzi wa kampuni ya vinywaji ya jambo Esme Salum, pamoja na wachezaji wa timu ya Stand United na wachekeshaji kutoka Futuhi, wakipiga picha ya pamoja na watoto wenye ualbino cha Buhangija.
Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post