IRAN YAGOMA KUKABIDHI KISANDUKU CHEUSI CHA NDEGE YA UKRAINE ILIYOIPIGA KOMBORA KWA BAHATI MBAYA

Kisanduku cheusi cha ndege ya abiria ya Ukraine iliyoangushwa kwa bahati mbaya nchini Iran mwezi uliopita kimeharibika lakini Iran haitakabidhi kisanduku hicho kwa nchi nyingine licha ya shinikizo la kufanya hivyo, mawaziri wa ngazi ya juu wa Iran wamesema , kwa mujibu wa vyombo vya habari vya taifa hilo. 

Waziri mkuu wa canada Justin Trudeau alisema wiki iliyopita kuwa amemshauri waziri wa mambo ya kigeni wa Iran Mohammad Javad Zarif kuwa uchunguzi kamili na huru kuhusiana na kudunguliwa kwa ndege hiyo ni lazima ufanyike. 

Wengi wa abiria 176 waliofariki katika mkasa huo ni Wairani wenye uraia pacha, ambao hautambuliki na Iran. 

Canada ilikuwa na raia 57 katika ndege hiyo. Waziri wa ulinzi wa Iran Amir Hatami alisema kisanduku hicho cha kurekodia data za safari, kimeharibika na kiwanda cha jeshi kimeombwa kusaidia katika kukikarabati.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527