RC MTAKA : ‘FAHARIKILIMO MKOMBOZI WA WAKULIMA WA PAMBA’




Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akitoa hotuba yake wakati wa Kongamano la Wadau wa Sekta ya Kilimo lililoandaliwa na Benki ya CRDB kwa kushirikiana na Shirika la Uwezeshaji Sekta ya Kilimo (PASS). Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Mikopo wa Benki ya CRDB, Xavery Makwi na Meneja wa Kanda ya Ziwa Benki ya CRDB, Lusingi Sitta.


Na Mwandishi Wetu 

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka amesema akaunti ya FahariKilimo ya Benki ya CRDB imekuwa mkombozi mkubwa kwa wakulima wa Pamba Kanda ya Ziwa Victoria.

Mtaka alisema huduma zinazoambatana na akaunti ya FahariKilimo ikiwamo mikopo ya pembejeo na zana za kilimo zimesaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza tija kwa wakulima pamoja na kuboresha mnyororo wa thamani wa kilimo nchini.


Mtaka amesema hayo Februari 10,2020 wilayani Bariadi mkoani Simiyu wakati wa kongamano la wadau wa sekta ya kilimo lilioandaliwa na Benki ya CRDB kwa kushirikiana na Shirika la Uwezeshaji Sekta ya Kilimo (PASS).

Akitoa hotuba yake katika kongamano hilo ambalo lililohusisha wadau wa pamba kutoka mikoa ya Simiyu, Mwanza na Mara, Malima aliipongeza Benki ya CRDB kwa kutoa zaidi ya shilingi bilioni 100 kwa ajili ya kuboresha kilimo cha Pamba.


“Sote tunafahamu changamoto ambayo tuliipata katika zao la Pamba mwaka jana, lakini Benki ya CRDB ilionyesha uzalendo wa hali ya juu kwa kushirikiana na Serikali kutoa mikopo kwa wanunuzi wa Pamba lakini pia kutafuta masoko ndani na nje ya nchi, hili ni jambo la kupongezwa sana,” alisema Mtaka.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mara ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uendelezaji zao la Pamba, Adam Malima, alisema Serikali inaridhishwa na jitihada kubwa zinazofanywa na Benki hii ya CRDB katika kuboresha sekta ya kilimo nchini.

Malima alisema Serikali ya Awamu ya Tano imejidhatiti katika kuhakikisha zao la Pamba linaongezeka thamani ili kuboresha maisha ya wakulima wa Pamba.

“Niwaombe wakulima wetu wa Pamba tuendelee kutumia fursa hizi zinazotolewa na Benki yetu ya CRDB, tukifanya hivyo tutaweza kuongeza uzalishaji na kuongeza thamani ya kilimo chetu. Serikali ipo tayari kufanya kazi bega kwa bega na Benki ya CRDB kuhakikisha tunafikia malengo tuliyojiwekea,” alisema Malima.

Mkurugenzi wa Mikopo wa Benki ya CRDB, Xavery Makwi, alisema akaunti ya FahariKilimo ni sehemu ya mkakati mpana wa benki kuwahudumia wakulima kwa ukaribu zaidi kwa kuzingatia mahitaji yao.

Makwi alisema mpaka sasa wakulima zaidi ya 30,000 tayari wameshajiunga na akaunti ya FahariKilimo na hivyo kunufaika na fursa mbalimbali zinazotolewa na Benki ya CRDB.

“Akaunti hii ya FahariKilimo hufunguliwa bure kabisa na hakuna gharama zozote za uendeshaji wa akaunti kwa mkulima, tukilenga kumpa mkulima unafuu wa kupokea malipo yake pindi anapopokea malipo baada ya kuuza mazao,” alisema Makwi.

Makwi alisema wakulima ambao wamejiunga na FahariKilimo wameweza kunufaika na mikopo ya pembejeo, mikopo ya zana za kilimo, mikopo ya ujenzi wa maghala, pamoja na uunganishwaji na masoko. “Uwezeshaji huu tunaufanya pia katika uwekezaji katika viwanda vya uchenjuaji Pamba.

Makwi alisema baadhi ya viwanda vilivyonufaika na uwezeshaji huu unaofanywa na Benki ya CRDB ni pamoja na Gaki Investment Company Ltd, Fresho Investment Company Ltd, Aham Investment Company Ltd, Nsagali Company Ltd na Birchand Oil Mill Limited.

Meneja wa PASS Kanda ya Ziwa, Langelika Kalebi alisema shirik a hilo litaendelea kushirikiana na Benki ya CRDB kuwawezesha wakulima na vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) wa Pamba hususani katika kuandaa mpango wa kilimo na uongezaji wa thamani wa dhamana ikiwa ni vitu muhimu vinavyohitajika wakati wa uombaji wa mikopo ya pembejeo, zana za kilimo na maghala.

Akiongea kwa niaba ya wakulima wa Pamba, Medard Marko mkulima wa Pamba kutoka wilaya ya Bariadi vijijini ameishukuru Benki ya CRDB kwa kuwa mkombozi kwa wakulima kupitia akaunti ya FahariKilimo.
“Kupitia akaunti hii tumekuwa tukipata mafunzo ya mara kwa mara juu ya uboreshwaji wa kilimo chetu, lakini pia tumekuwa tukiunganishwa na huduma za mikopo ya pembejeo, zana za kilimo kama matrekta na ujenzi wa maghala kupitia AMCOS,” alisema Marko. 

Takwimu zinaonyesha mkoa wa Simiyu unaongoza nchini kwa uzalishaji wa zao la Pamba, akizungumza katika kongamano hilo Afisa Kilimo wa Wilaya ya Bariadi vijijini, Golong’a Ally alisema mwaka jana mkoa huo pekee umezalisha zaidi ya kilo milioni 160 za Pamba.

ANGALIA MATUKIO KATIKA PICHA
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima wakiwasili katika Kongamano la Wadau wa Sekta ya Kilimo lililoandaliwa na Benki ya CRDB kwa kushirikiana na Shirika la Uwezeshaji Sekta ya Kilimo (PASS).
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akitoa hotuba yake wakati wa Kongamano la Wadau wa Sekta ya Kilimo lililoandaliwa na Benki ya CRDB kwa kushirikiana na Shirika la Uwezeshaji Sekta ya Kilimo (PASS). Wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mara na Mwenyekiti wa Kamati ya Uendelezaji wa zao la Pamba, Adam Malima.
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima akitoa hutuba yake wakati wa Kongamano la Wadau wa Sekta ya Kilimo lililoandaliwa na Benki ya CRDB kwa kushirikiana na Shirika la Uwezeshaji Sekta ya Kilimo (PASS).
Meneja wa Kanda ya Ziwa Benki ya CRDB, Lusingi Sitta akielezea fursa mbalimbali zinazotolewa na Benki ya CRDB kwa wakulima wa Pamba wakati wa  Kongamano la Wadau wa Sekta ya Kilimo lililoandaliwa na Benki ya CRDB kwa kushirikiana na Shirika la Uwezeshaji Sekta ya Kilimo (PASS).
Mkurugenzi wa Mikopo Benki ya CRDB, Xavery Makwi akizungumza katika  Kongamano la Wadau wa Sekta ya Kilimo lililoandaliwa na Benki ya CRDB kwa kushirikiana na Shirika la Uwezeshaji Sekta ya Kilimo (PASS).
Wadau wa pamba wakiwa kwenye  Kongamano la Wadau wa Sekta ya Kilimo lililoandaliwa na Benki ya CRDB kwa kushirikiana na Shirika la Uwezeshaji Sekta ya Kilimo (PASS).

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga akizungumza na wadau wa Pamba waliohudhuria katika Kongamano la Wadau wa Sekta ya Kilimo lililoandaliwa na Benki ya CRDB kwa kushirikiana na Shirika la Uwezeshaji Sekta ya Kilimo (PASS).


Wadau wa pamba wakiwa ukumbini.

Mkurugenzi wa Kampuni ya uchenjuaji Pamba Nsagali Ltd, Gungu Silanga akielezea namna ambavyo kampuni hiyo imenufaika na mikopo ya uwezeshaji kwa viwanda inayotolewa na Benki ya CRDB.

Wadau wa pamba wakiwa ukumbini.
Wadau wa pamba wakiwa kwenye kongamano hilo.

Kongamano likiendelea.
Afisa Kilimo wa Wilaya ya Bariadi vijijini, Golang'a Ally akitoa maelezo ya kilimo cha Pamba katika wilaya yake.
Mmoja wa wadau wa zao la Pamba akichangia mada wakati wa Kongamano hilo.
Mmoja wa wadau wa zao la Pamba akichangia mada wakati wa Kongamano hilo.
Wakulima wa zao la Pamba wakiendelea na zoezi la ufunguaji akaunti wakati wa  Kongamano la Wadau wa Sekta ya Kilimo lililoandaliwa na Benki ya CRDB kwa kushirikiana na Shirika la Uwezeshaji Sekta ya Kilimo (PASS).
Awali wakulima wakijisajili kabla ya kuanza kwa kongamano hilo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527