WANAJESHI NA POLISI WAVAMIA BUNGE WAKISHINIKIZA KUPEWA MKOPO WANUNUE VIFAA VYA KUDHIBITI UHALIFU

Wanajeshi na maafisa wa polisi waliojihami nchini El Salvador wamevamia bunge , wakitaka kuidhinishwa kwa mkopo wa dola milioni 109 ili kuwanunulia vifaa vya kukabiliana na uhalifu.

Waliingia katika jengo la bunge wakati rais Nayib Bukele alipokuwa anakaribia kuwahutubia wabunge .

Siku ya Ijumaa aliwapatia siku saba za kuunga mkono mpango wake wa kuchukua mkopo. Viongozi wa upinzani walitaja uvamizi huo wa wanajeshi bungeni kuwa kama kitendo cha kutishia.

Taifa la El salvador lina viwango vya juu vya mauaji duniani. Ghasia nyingi hutekelezwa na magenge ya uhalifu ambayo hufanya kazi katika eneo la Marekani ya kati.

Rais Bukele ambaye alichukua mamlaka mnamo mwezi Juni 2019 , anataka kutumia mkopo huo kuimarisha vifaa vya maafisa wa polisi na wanajeshi katika vita dhidi ya uhalifu.President Nayib Bukele addressed his supporters outside the parliament building

Ameahidi kukabiliana na ghasia zinazotekelezwa na wahalifu pamoja na ufisadi katika taifa hilo lenye viwango vya juu vya umasikini.

Siku ya Jumapili , mamia ya watu walikongamana nje ya bunge katika mji mkuu wa San Salvador kuunga mkono mpango wa usalama wa rais.
Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527