HATIMAYE BERNARD MEMBE AHOJIWA CCM ...."NIMEKUWA MTU WA FURAHA KUBWA YA AJABU"

Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema amekuwa mtu wa furaha baada ya kuhojiwa na Kamati ya Maadili ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), jijini Dodoma leo Alhamisi Februari 6,2020.

Membe amesema hayo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutoka katika mahojiano hayo yaliyochukua saa tatu.

“Tulikuwa na mkutano wa masaa matano ya mijadala mizuri, mikubwa, ya kitaifa inayohusu Chama chetu Cha Mapinduzi na nchi yetu, na nimekuwa mtu wa furaha kubwa ajabu kwa sababu nimepata nafasi nzuri ya kufafanua mambo kadhaa ambayo chama changu Kilitaka kuyajua.

“Nimepata nafasi ya kutoa mawazo ya yale mambo ambayo niliombwa kutoa, kwa hiyo sasa hivi mimi na mke wangu tunakwenda kula chakula kizuri sana kwenye hoteli moja ambayo haijulikani baada ya hapo nitaanza safari ya kurudi Dar es Salaam, lakini niwaambie safari hii ya kuja Dodoma, ilikuwa ni ya manufaa makubwa sasa sana kwa kwa chama na kwa taifa…” amesema Membe.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post