KAGERA SUGAR WAICHAPA YANGA 3 -0


Yusuph Mhilu mshambuliaji wa Kagera Sugar leo amekiongoza kikosi chake kuingamiza Yanga kwa mabao 3-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa leo, Januari,15, Uwanja wa Uhuru.

Mhilu alifungua akaunti ya mabao dakika ya 13 kwa kuachia shuti kali lililomshinda mlinda mlango Farouk Shikalo.

Yanga ikiwa chini ya nahodha wao Haruna Niyonzima kwenye mchezo wa leo ilimshuhudia kiungo wao Mohamed Issa 'Mo Banka' akiwapunguzia kasi dakika ya 44 baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu kutokana na kuonyeshwa kadi mbili za njano kwa kucheza faulo kwa wachezaji wa Kagera Sugar.

Kipindi cha kwanza Yanga walikwenda mapumziko wakiwa nyuma kwa bao 1-0 walijipanga kurejea kupindua meza kipindi cha pili mambo yakazidi kuwa magumu kwani Kagera Sugar iliyo chini ya Mecky Maxime ilimzidi ujanja Luc Eymael ambaye ni mara yake ya kwanza kukaa kwenye benchi la ufundi akipokea kijiti cha Mwinyi Zahera.

Bao la pili kwa Kagera Sugar lilifungwa dakika ya 66 kupitia kwa Ally Ramadhan aliyemalizia pasi ya Abdallah Siseme na msumari wa mwisho ulipachikwa kwa kichwa dakika ya 89 na kuifanya Yanga kushindwa kutumia dakika nne za nyongeza kupata bao la kufutia machozi.

Kagera Sugar imecheza jumla ya mechi 17 inafikisha jumla ya pointi 27 inapanda mpaka nafasi ya nn, Yanga inakuwa nafasi ya nane ikiwa imecheza jumla ya mechi 13 na ina pointi 25 kibindoni.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post