WAOMBOLEZAJI WAFARIKI KATIKA MKANYAGANO WAKATI WA MAZISHI YA JENERALI WA IRAN ALIYEUAWA NA MAREKANI

Karibu watu 35 wameripotiwa kufarika kufuatia kisa cha mkanyagano katika mazishi ya Qasem Soleimani, jenerali wa kikosi maalum cha jeshi la Iran aliyeuawa na Marekani wiki iliyopita.

Zaidi ya watu 40 pia wamejeruhiwa katika kisa hicho kilichotokea mjini Kerman, kwa mujibu wa ripoti hizo.

Qasem Soleimani anazikwa leo nyumbani kwake ambako mamilioni ya watu wamekusanyika  barabarani kumuaga.

Mauaji yake yameibua hofu ya kuzuka kwa mzozo kati ya Marekani na Iran.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527