IRAN YAIWEKA WIZARA YA ULINZI YA MAREKANI KWENYE ORODHA YA KUNDI LA KIGAIDI....YAONGEZA BAJETI KWENYE JESHI LAKE LA QUDS

Shirika la habari la Iran limesema, bunge la nchi hiyo leo limeitaja wizara ya ulinzi ya Marekani kuwa ni kundi la kigaidi.


Habari zinasema, kwa mujibu wa kura zilizopigwa na wabunge wa Iran, idara zote na kampuni zenye ushirika na wizara ya ulinzi ya Marekani, na makamanda wa Marekani waliopanga na kumuua aliyekuwa kamanda wa kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC Bw. Qassem Soleimani, wamewekwa kwenye orodha ya kundi la kigaidi. 


Kadhalika, Kiongozi Mkuu wa Iran  Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ameidhinisha kukiongeza Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) Yuro milioni 200.
 


Khamenei, jana usiku aliidhinisha kutolewa fedha hizo kutoka kwenye Hazina ya Maendeleo ya Taifa kwa ajili ya Kikosi cha Quds cha SEPAH.

Aidha katika kikao hicho cha leo, Wabunge wa Iran wamepitisha kwa kauli moja hoja ya "Kulipa Kisasi ' ambayo itaandaa mazingira kwa Iran kulipiza kisasi dhidi ya Marekani  kwa kumuua Jenerali Qasse Soleimani, aliyekuwa Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Quds


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527