TUME YA VYUO VIKUU -TCU YAVIFUTIA USAJILI VYUO 9 TANZANIA

Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) imefuta hati za usajili wa vyuo vikuu vishiriki vitano, vyuo vikuu vitatu na chuo kikuu kishiriki kimoja.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Januari 21, 2020 jijini Dar es Salaam katibu mtendaji wa TCU, Profesa Charles Kihampa amesema vyuo hivyo vimeshindwa kujirekebisha na hata vingepewa muda zaidi visingeweza.

Amesema vyuo vishiriki ni Chuo kikuu kishiriki cha Askofu Mkuu Yakobo (AJUCO), Chuo Kikuu cha kumbukumbu ya Kardinali Rugambwa (CARUMUCo) na Chuo kikuu cha Theofilo Kisanji (Teku- Dar es Salaam), Chuo kikuu cha Mtakatifu Yohana cha Tanzania kituo cha St Marks na Chuo kikuu cha Jomo Kenyatta cha Kilimo tawi la Arusha (JKUA).

TCU pia imefuta hati za usajili wa vyuo vitatu ambavyo ni Chuo kikuu cha Josiah Kibira (Kagera), Mount Meru (Arusha), IMTU (Dar es Salaam). Chuo kikuu kishiriki kilichofutiwa usajili ni Chuo Kikuu cha Bagamoyo (Pwani).

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527