BENKI YA TPB YATOA ELIMU KWA WALIMU WASTAAFU WILAYANI KAHAMA



Benki ya TPB  imetoa elimu kwa walimu wastaafu wilayani kahama kuhusu maboresho ya huduma zao lakini namna gani mzee anapaswa kuwekeza na kuwa na matumizi bora ya pesheni yake.

Akizungumza katika mkutano huo Januari 4,2020  Meneja wa Benki ya TPB mkoa wa Shinyanga Jumanne Wagana
aliwapa wazee Elimu  ya BIMA ya Maisha ya Tsh 1000/=, Biashara ya akaunti ya Amana kwa muda maalumu inayokupa faida mpaka 12%,  jinsi ya kupata mitaji kupitia mikopo ya riba nafuu ya wastaafu, mikopo ya kilimo, mikopo ya biashara n.k.

 Katika mkutano huo ambao ulifadhiliwa na Benki ya TPB wastaafu mbalimbali walitoa shukrani zao za dhati kwa Benki ya Serikali ya TPB kwa kuwajali na kuwawezesha wafikie malengo yao ambayo walikuwa hawajakamilisha wakati wanastaafu. 

Naye Kaimu Meneja wa tawi la Kahama  Patrice Garani  akichangia amewaomba wazee wasiogope kukopa kwani mikopo ya TPB ina Bima.
Meneja wa TPB Mkoa wa Shinyanga Ndg Jumanne Wagana akitoa Elimu kwa Waalimu Wastaafu wilayani ya Kahama.
Walimu Wastaafu wakifuatilia kwa umakini Wawezeshaji kutoka Benki ya TPB wakitoa elimu ya fedha, mikopo na ujasiriamali.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post