TAHADHARI YA MVUA KUBWA NA UPEPO KWA SIKU 5


Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya mvua kubwa na upepo mkali katika baadhi ya maeneo ya Mikoa ya Lindi, Mtwara, Dar es Salaam, Zanzibar na Pwani kwa muda wa siku tano kuanzia jana.



Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, kuanzia jana hadi Jumapili, kunatarajiwa kuwapo upepo mkali na mawimbi makubwa kwa baadhi ya maeneo ya Pwani ya Bahari ya Hindi, hivyo kusababisha shida kwenye uvuvi na usafiri wa baharini.

"Kiwango cha mvua na upepo ni cha wastani, hivyo wananchi wachukue tahadhari katika shughuli zao," TMA ilieleza katika taarifa yake hiyo.

Ilisema athari huenda zikajitokeza kutokana na kusimama kwa shughuli za binadamu, kuharibika kwa miundombinu na makazi kuzingirwa na maji, hivyo kuna haja kuchukua tahadhari.

Mamlaka hiyo ilisema mvua inayonyesha sasa ni mwendelezo wa utabiri wa mvua za vuli ilioutoa kipindi cha nyuma na katika baadhi ya maeneo itaendelea hadi mwezi ujao.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post