NZIGE WATAFUNA HEKTA 70,000 ZA MASHAMBA KENYA, SOMALIA NA ETHIOPIA...RWANDA YAWEKA TAHADHARI


Rwanda iko kwenye tahadhari ya hali ya juu kufuatia uvamizi wa nzige unaoweza kutokea ambao kwa sasa wameonekana katika nchi kadhaa za Afrika Mashariki, zikiwemo Ethiopia, Kenya na Somalia. 


Waziri wa kilimo na rasilimali ya wanyama wa Rwanda Bibi Geraldine Mukeshimana amesema, wizara yake iko tayari kukabiliana na uvamizi huo wa nzige. 

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa limesema, nzige wameharibu karibu hekta 70,000 za mashamba nchini Somali na Ethiopia, na kutishia utoaji wa chakula katika nchi hizo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post