Picha : WADAU WA MAJI KUTOKA TABORA WATEMBELEA SHUWASA KUJIFUNZA MBINU ZA KUENDESHA MRADI WA MAJI YA ZIWA VICTORIA


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Wadau wa Maji zaidi ya 80 kutoka mkoani Tabora leo Januari 15,2020 wametembelea Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) kwa ajili ya kujifunza mbinu za kuendesha mamlaka za maji na kuendesha Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria ambao hivi karibuni utaanza kuwanufaisha wananchi wa Tabora.


Wadau hao wametembelea chanzo cha Maji cha Bwawa la Ning’hwa kilichopo katika kata ya Chibe Manispaa ya Shinyanga na namna wanavyotibu maji hayo sambamba na kujionea Tenki la maji lililopo kata ya Old Shinyanga lenye ujazo wa mita za ujazo 18,000 linalopokea maji kutoka kwenye Tenki la Mabale ambalo lina maji ya Ziwa Victoria.

Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira katika mji wa Kahama na Shinyanga (Kahama Shinyanga Water Supply and Sanitation Authority (KASHWASA) ndiyo inatekeleza mradi wa Maji ya Ziwa Victoria na kuyasambaza kwenye maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na kuuza maji hayo kwenye mamlaka za maji ikiwemo SHUWASA na sasa inapeleka mradi wa maji mkoani Tabora.

Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA,Flaviana Kifizi alisema wanategemea maji kutoka vyanzo vikuu viwili ambavyo ni Bwawa la Ning’hwa na Maji ya Ziwa Victoria kupitia KASHWASA.

“Kutokana na changamoto za upatikanaji na uzalishaji wa majisafi kutoka Bwawa la Ning’hwa na kwa kuzingatia uwekezaji wa serikali katika mradi unaosimamiwa na KASHWASA. Mwaka 2009 SHUWASA iliamua kuanza kutumia maji kutoka KASHWASA ili kutatua changamoto za upatikanaji na uzalishaji wa maji katika Manispaa ya Shinyanga na kutufanya kuwa na chanzo cha uhakika cha maji”,alifafanua Kifizi.

Alisema licha ya kufanikiwa kuwafikishia wananchi wa Manispaa ya Shinyanga huduma ya maji safi kwa asilimia 80.3 kutokana na maji ya KASHWASA,wanakabiliwa na changamoto ya gharama kubwa ya uzalishaji,mgandamizo mkubwa wa maji kutoka Ziwa Victoria unaosababisha miundombinu kupasuka mara kwa mara na kusababisha gharama za uendeshaji kuongezeka.

“Changamoto nyingine ni umbali mkubwa baina ya vifaa vya kudhibiti maji ‘control valves’ katika mabomba makubwa hali inayosababisha kupotea kwa maji mengi wakati wa matangazo”,alieleza Kifizi.

Aidha alisema uhaba wa vitendea kazi bado ni tatizo pamoja na uhaba wa mabomba na viungio vyake kwa ajili ya matengenezo ‘spare pipes and fittings’.

Kifizi alizikumbusha Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira Tabora,Nzega na Igunga (TUWASA,NZUWASA na IGUWASA) kutambua kuwa mradi wa Maji ya Ziwa Victoria ni mkubwa hivyo kujipanga vizuri ili kukabiliana na changamoto za uendeshaji wa mradi huo.

Naye Kaimu Tawala Msaidizi mkoa wa Tabora,Rukia Manduta alisema pindi maji yatakapofika mkoani Tabora watajitahidi kupanga bei za maji zinazoendana na kipato cha wananchi.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Tabora Leopard alisema ziara hiyo imewasaidia kupata elimu ya kutosha kuhusu namna ya kuendesha mamlaka za maji lakini pia jinsi ya kutekeleza kwa ufanisi mradi wa maji ya Ziwa Victoria.

Nao Mkuu wa wilaya ya Nzega, Godfrey Ngupula na wilaya ya Igunga,John Mwaipopo walisema wapo tayari kupokea mradi wa maji ya Ziwa Victoria mkoani Tabora ambapo tayari Maji yamefika katika Tenki la Ushirika lililopo Nzega kwa ajili ya majaribio.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA,Flaviana Kifizi akielezea namna Bwawa la Ning'wa linavyosaidia wananchi wa Manispaa ya Shinyanga kupata huduma ya maji safi wakati Wadau wa Maji kutoka Mkoa wa Tabora walipotembelea Bwawa la Ning'wa lililopo katika kata ya Chibe ili kujionea namna uzalishaji na usambazaji wa maji unavyofanyika. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Muonekano wa sehemu ya bwawa la Ning'wa.
Meneja Ufundi wa SHUWASA,Mhandisi Yusuph Katopola akielezea kuhusu bwawa la Ning'hwa lililojengwa mwaka 1972 na kufanyiwa ukarabati mwaka 1984 na lilipokauka mwaka 2000 wakaanzisha mradi wa Visima ili kuwapatia huduma ya maji wakazi wa Shinyanga.
Wadau wa maji kutoka mkoa wa Tabora wakiondoka katika bwawa la Ning'hwa ambalo ni chanzo cha maji kwa SHUWASA.
Mkuu wa wilaya ya Igunga,John Mwaipopo (mbele) na Mkuu wa wilaya ya Nzega, Godfrey Ngupula wakiwa na wadau wa maji mkoa wa Tabora wakitembelea eneo la kutibu maji ya bwawa la Ning'hwa na kuangalia namna maji hayo yanavyochujwa kabla ya kusafirishwa kwenda kwa wananchi.
Wadau wa maji mkoa wa Tabora wakitembelea eneo la kutibu maji ya bwawa la Ning'hwa. Mbele ni Katibu Tawala Msaidizi mkoa wa Tabora,Rukia Manduta.
Wadau wa maji wa mkoa wa Tabora wakitembelea eneo la kutibu maji ya bwawa la Ning'hwa.
Wadau wa maji mkoa wa Tabora wakitembelea eneo la kutibu maji ya bwawa la Ning'hwa.
Wadau wa maji mkoa wa Tabora wakitembelea eneo la kutibu maji ya bwawa la Ning'hwa.
Katibu Tawala Msaidizi mkoa wa Tabora,Rukia Manduta (katikati) akiwa na Mkuu wa wilaya ya Igunga,John Mwaipopo (kushoto) na Mkuu wa wilaya ya Nzega, Godfrey Ngupula (kulia) katika eneo la kutibu maji ya bwawa la Ning'hwa.
Wadau wa maji kutoka mkoa wa Tabora wakiwa katika eneo la kutibu maji ya bwawa la Ning'hwa.
Muonekano wa mitambo inayotumika kusukuma maji ya Bwawa la Ning'hwa kwenda kwenye matenki tayari kwa ajili ya kuwafikia wananchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA,Flaviana Kifizi akionesha Tenki la Maji ya Ziwa Victoria lililopo katika kata ya Old Shinyanga.Tenki hilo linalomilikiwa na SHUWASA ndiyo linapokea maji kutoka KASHWASA.
Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA,Flaviana Kifizi akiwaelezea wadau wa maji kutoka Tabora jinsi wanavyonunua maji kutoka KASHWASA na kuyauza kwa wananchi wa Manispaa ya Shinyanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA,Flaviana Kifizi akiwaelezea wadau wa maji kutoka Tabora jinsi wanavyonunua maji kutoka KASHWASA na kuyauza kwa wananchi wa Manispaa ya Shinyanga.
Mjumbe wa Bodi ya SHUWASA, Ziporah Pangani akifafanua jambo kwa wadau wa maji kutoka mkoa wa Tabora.
Muonekano wa tenki la SHUWASA linalopokea maji kutoka KASHWASA.
Wadau wa maji kutoka mkoa wa Tabora wakiondoka katika tenki la SHUWASA.
Wadau wa maji kutoka mkoa wa Tabora wakiangalia tenki dogo la maji linalotumika kusambaza Maji katika Manispaa ya Shinyanga.
Afisa Mahusiano wa SHUWASA,Nsianel Gelard akisoma taarifa ya SHUWASA kwa wadau wa maji kutoka mkoa wa Tabora wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara ya wadau hao wa maji kutoka mkoa Tabora leo Januari 15,2020 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga.
Afisa Mahusiano wa SHUWASA,Nsianel Gelard akisoma taarifa ya SHUWASA kwa wadau wa maji kutoka mkoa wa Tabora.
Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA,Flaviana Kifizi akizungumza wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara ya wadau wa maji kutoka mkoa Tabora leo Januari 15,2020 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA,Flaviana Kifizi akizungumza wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara ya wadau wa maji kutoka mkoa Tabora leo Januari 15,2020 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga.
Katibu Tawala Msaidizi mkoa wa Tabora,Rukia Manduta akizungumza wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara ya wadau wa maji kutoka mkoa Tabora leo Januari 15,2020 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga.
Wadau wa maji kutoka Tabora wakiwa ukumbini.
Wadau wa maji kutoka Tabora wakiwa ukumbini.
Wadau wa maji kutoka Tabora wakiwa ukumbini.
Wadau wa maji kutoka Tabora wakiwa ukumbini.
Mkurugenzi wa KASHWASA,Mhandisi Joshua Mgeyekwa akizungumza wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara ya wadau wa maji kutoka mkoa Tabora leo Januari 15,2020 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Igunga, John Mwaipopo akizungumza wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara ya wadau wa maji kutoka mkoa Tabora leo Januari 15,2020 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Nzega Godfrey Ngupula akizungumza wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara ya wadau wa maji kutoka mkoa Tabora leo Januari 15,2020 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Tabora Leopard  akizungumza wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara ya wadau wa maji kutoka mkoa Tabora leo Januari 15,2020 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga.
Wadau wa maji wakiwa ukumbini.
Wadau wa maji wakiwa ukumbini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post