TAARIFA YA ONGEZEKO LA HALI YA JOTO KWA BAADHI YA MAENEO NCHINI





Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema kutakua na ongezeko la joto katika baadhi ya maeneo nchini, kufuatia kuwepo kwa hali ya unyevunyevu angani.

TMA imeyataja maeneo yatakayoathirika zaidi ni ukanda wa pwani yanayotarajiwa kuwa na kiwango cha juu cha joto cha nyuzi joto 32 hadi 34 hususan kwa maeneo ya Dar es Salaam, Tanga, Unguja na Pemba.

Taarifa kwa umma iliyotolewa jana Jumanne, Januari 7, 2020 na Mkurugenzi Mkuu TMA, Dk Agnes Kijazi imeeleza kwa kawaida kipindi cha Oktoba hadi Machi kila mwaka 2020 jua la utosi linakuwa katika maeneo ya kizio cha kusini mwa dunia.

Amesema Tanzania ikiwa ni moja ya nchi zilizopo katika kizio cha kusini, huwa na hali ya joto kali katika maeneo mengi ikilinganishwa na miezi mingine.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527