SPIKA NDUGAI ATAKA HATUA ZA HARAKA ZICHUKULIWE KUSAIDIA WAATHIRIKA WA MAFURIKO LINDI


Mvua zinazoendelea kunyesha katika mikoa mbalimbali zimesababisha maafa makubwa ikiwemo watu wanne kupoteza maisha na watu zaidi ya 661 katika vijiji zaidi ya sita wakikosa makazi ya kuishi katika mikoa ya Lindi na Iringa.

Pamoja na hayo, miundombinu ikiwemo madaraja na mashamba imeharibiwa vibaya na mvua hizo.

Mkoani Lindi watu 600 kutoka vijiji vya Mikole, Kipindimbi, Makanganga Mitolea wilayani Kilwa jana wameokolewa kwa njia ya boti baada ya kuzungukwa na maji yatokanayo na mvua zinazoendelea kunyesha.


Leo January 28, 2019  Spika wa Bunge, Job Ndugai amezungumzia hali ya mafuriko hayo hasa mkoani Lindi na kutaka ofisi ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) kuchukua hatua za haraka katika kusaidia waathirika wa mafuriko hayo ambayo yamesababisha vifo vya watu nane hadi sasa.

“Ni kweli mvua inanyesha karibu kila mahali nchi nzima lakini kwa taarifa tulizo nazo hivi sasa ni kwamba katika Mkoa wa Lindi katika jimbo la Waziri Mkuu kule Luangwa kuna mafuriko kwahiyo tunakuomba sana Waziri wa nchi uweze kuona hali hiyo,” – Amesema Spika wa Bunge, Job Ndugai leo Bungeni


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527