BARUA YA RAIS MAGUFULI YATUA BUNGENI DODOMA


Spika wa Bunge Job Ndugai amesema Rais Magufuli amepokea azimio la pongezi lililofikiwa na Bunge kwenye kikao cha 17, kufuatia mafanikio na mageuzi kwenye utendaji kazi wa Serikali na pia ameandika barua ya kulishukuru Bunge kwa kutambua mchango wake.


Barua hiyo ya Rais imesomwa kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 18 na Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai  ambapo amesema Rais Magufuli analishukuru Bunge kwa kutambua mchango wake wa kuliletea maendeleo Taifa.

“Niendelee kuwaasa Wabunge na watanzania kwa ujumla tuendelee kuipambania nchi yetu, ili tuweze kufikia maendeleo yenye uchumi wa kati” amesema Spika Ndugai wakati akisoma barua ya Rais Magufuli.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527