SERIKALI YASEMA HAKUNA MTANZANIA YEYOTE CHINA AMEKUMBWA NA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA CORONA | MALUNDE 1 BLOG

Monday, January 27, 2020

SERIKALI YASEMA HAKUNA MTANZANIA YEYOTE CHINA AMEKUMBWA NA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA CORONA

  Malunde       Monday, January 27, 2020

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi, amesema kuwa hakuna Mtanzania yeyote anayeishi nchini China, aliyekumbwa na maambukizi ya virusi vya homa ya Corona, vilivyozuka katika Mataifa ya Marekani, China, Thailand, Korea Kusini na Japan.

Waziri Kabudi ameyasema hayo wakati akitoa ufafanuzi juu ya hali ya Watanzania waishio nchini China na kusema kuwa Tanzania ina wanafunzi takribani 4000, ambapo katika mji wa Wuhan kuna wanafunzi 400 na kwamba kwa mujibu wa Balozi wa Tanzania Nchini China, Balozi Mbelwa Kairuki, ameihakikishia Serikali kuwa mpaka sasa hakuna mtanzania yeyote aliyeathiriwa ama kukumbwa na maradhi hayo.

Ameongeza kuwa Tanzania inaendelea kufuatilia kwa ukaribu kujua maendeleo na hali za Watanzania wanaoishi jimboni Wuhan na China kwa ujumla na kuwataka Watanzania kuwa makini na suala la kutoa taarifa zisizo rasmi ama uvumi, kwani kwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria za Tanzania na kuwataka kuwa na subira ili kupata taarifa rasmi kutoka serikalini.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post