KAULI YA SIMBACHAWENE BAADA YA KUAPISHWA KUWA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI


Waziri wa Mambo ya Ndani  George Simbachawene ameahidi kushirikiana na viongozi wengine kuleta matokeo chanya yanayotarajiwa na Watanzania.


Simbachawene ameapishwa leo Jumatatu Januari 27, 2020 Ikulu, Dar es Salaam baada ya kuteuliwa na Rais Magufuli kuongoza wizara hiyo akichukua nafasi ya Kangi Lugola ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Simbachawene amesema ataviheshimu vyombo vya usalama kufanya kazi yake huku yeye akishughulika na mambo ya utawala.

“Pale ambapo vyombo vinafanya makosa kazi yangu ni kukutaarifu kwamba kuna mambo hayapo sawa, lakini mimi sina cheo chochote na wala sina nyota yoyote na hukunipa nyota hapa lao.”

“Umenipa jukumu nikusaidie katika kusimamia vyombo hivi ambavyo kwa sehemu vinafanya kazi ya ulinzi na usalama na ninatambua mimi sio amiri jeshi mkuu,” amesema Simbachawene


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527