PROFESA LIPUMBA AKAMATWA NA JESHI LA POLISI | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, January 26, 2020

PROFESA LIPUMBA AKAMATWA NA JESHI LA POLISI

  Malunde       Sunday, January 26, 2020

Jeshi la Polisi wilayani Handeni mkoani Tanga, limemkamata Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba, kwa madai ya kufanya ziara bila kuwa na kibali. Profesa Lipumba amekamatwa leo Jumapili Januari 26, 2020 Kijiji cha Segera wilayani Handeni na kupelekwa kituo kikuu cha polisi wilayani humo kilichopo mjini Handeni.

Mkurugenzi wa Usalama wa CUF, Masoud Mhina amesema mwenyekiti huyo amekamatwa wakati akijiandaa kufungua tawi la chama hicho Kijiji cha Segera.

Amesema ameshangazwa na kitendo hicho cha polisi kumkamata Profesa Lipumba wakati tayari chama kilishawasilisha jeshi la polisi taarifa ya ziara hiyo.


Taarifa zaidi zitafuata, juhudi za kumtafuta RPC Tanga zinaendelea.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post