MWANAMKE AFARIKI DUNIA BAADA YA KUPIGWA NA MME WAKE

Na Amiri Kilagalila-Njombe

Jeshi la polisi mkoani Njombe linamshikilia ndugu Josphat Mtega (24) mkazi wa Ramadhani mjini Njombe kwa tuhuma za kumsababishia kifo  mkewe kilichotokana na ugomvi.

Akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake,kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema mtuhumiwa huyo anashikiliwa na jeshi la polisi kutokana na kugombana na mkewe Angelina Sanga (24)  ambapo inadaiwa alimpiga na hivyo kumsababishia majeraha makubwa yaliyosababisha kifo chake.

Kamanda amesema mara baada ya ugomvi huo, Angelina alisafirishwa hadi hospitali ya Ikonda iliyopo wilayani Makete  ambapo baada ya kufikishwa katika hospitali hiyo uchunguzi wa kitabibu ulibaini kuwa dada huyo alionekana amevunjika mkono na sehemu mbali mbali za mwili wake zilionekana zimeshambuliwa vibaya.

Amesema mwanaume  huyo anaendelea kushikiliwa  na jeshi la polisi  kwa uchunguzi zaidi huku taratibu za kisheria zikiendelea.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527