KILICHOENDELEA MAHAKAMANI KATIKA KESI YA MUME ANAYETUHUMIWA KUMUUA MKEWE KWA KUMCHOMA MOTO | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, January 28, 2020

KILICHOENDELEA MAHAKAMANI KATIKA KESI YA MUME ANAYETUHUMIWA KUMUUA MKEWE KWA KUMCHOMA MOTO

  Malunde       Tuesday, January 28, 2020

Upande wa utetezi katika kesi inayomkabili Mfanyabishara Hamisi Luongo anayetuhumiwa kumuua Mkewe na kumchoma kwa gunia la mkaa, umeutaka upande wa mashtaka kukamilisha uchapishaji wa jarada la kesi hiyo ya mauaji ili shauri liendelee.

Hayo yamebainishwa na upande wa utetezi, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Salum Ally baada ya Wakili wa Serikali, Janeth Magoho kuieleza Mahakama ya Kisutu kuwa jarada halisi la shauri hilo lipo Polisi kwenye hatua ya kuchapwa.

“Shauri lilikuja kwa ajili ya kutajwa lakini jarada halisi lipo polisi kwenye hatua ya uchapishaji hivyo naiomba Mahakama hii iahirishe kesi hii”- Magoho.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Ally ameahirisha kesi hiyo hadi February,2020 litakapokuja kwa ajili ya kutajwa.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post